Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Mkutano wa kilele uliotarajiwa kuwakutanisha Waziri Mkuu wa India Narendra Modi na mwenzake wa Japan Shinzo Abe umeahirishwa.
Kulingana na wizara ya mambo ya kigeni ya India hatua hiyo inatokea wakati kukiwa na maandamano yaliyosababisha machafuko kwenye eneo lililoandaliwa kwa ajili ya mazungumzo.
Msemaji wa wizara hiyo Raveesh Kumar amesema kwenye taarifa yake kwamba pande zote zimeamua kuahirisha ziara hiyo hadi tarehe itakayokubalika katika siku za usoni.
Abe alitarajiwa kuwasili India Desemba 15 na kufanya mazungumzo na Modi katika mji wa Guwahati kaskazini mwa jimbo la Assam ambao hata hivyo umezingirwa na waandamanaji wiki hii wakipinga sheria mpya yenye utata kuhusu uraia.
Chanzo: DW Kiswahili