Mkutano wa siri kati ya Abdul Sykes na Jomo Kenyatta, Nairobi, 1950

Mkutano wa siri kati ya Abdul Sykes na Jomo Kenyatta, Nairobi, 1950

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
TUJIKUMBUSHE ILI TUJUE NA TUSISAHAU

KUTOKA MAKTABA: MKUTANO WA SIRI KATI YA ABDUL SYKES NA JOMO KENYATTA NAIROBI 1950

Siku moja katika mazungumzo na Ahmed Rashad Ali akanambia kuwa mwaka wa 1950 yeye akiwa Nairobi wakati wa mashindano ya Gossage Cup Abdul Sykes alifika Nairobi na akawa anakaa Railway Hotel.

Ahmed Rashad alikuwa nahodha wa timu ya Zanzibar.

Abdul alimfuata kwenye kambi yao akamwambia amekuja Nairobi kuonana na Jomo Kenyatta na akamtaka amsindikize.

Leo asubuhi katika pitapita yangu Maktaba nimeikuta taarifa ya Special Branch kuhusu mkutano wa Abdul Sykes na Jomo Kenyatta nami nakuwekeeni hapa barzani:

TAARIFA YA SIRI YA SPECIAL BRANCH KUHUSU MKUTANO WA ABDUL SYKES NA JOMO KENYATTA NAIROBI 1950

Hapo chini ni taarifa ya kikachero kuhusu harakati za TAA katika kutafuta ukombozi wa Tanganyika.

Document hii nliletewa kutoka Rhodes House Oxford.

Picha kulia ni Ahmed Rashad Ali aliyenieleza mkutano huu wa Abdul Sykes na Jomo Kenyatta na kushoto ni Jomo Kenyatta.

Abdul Sykes alikuwa kijana mdogo wa miaka 26.

Screenshot_20211008-113934_Facebook.jpg
 
Back
Top Bottom