Asante Left wing kwa ufafanuzi. Kesho tunamwua Goliath. Ndiyo atajua maana ya nguvu ya umma.
Naamini kuna watu wateleta Pucha hapa na ikiwezekana waweke Clip ya Maandamano baada ya Mkutano Mkuu mimi na Ktambi changu ilibidi niingie kwenye Maandamano maana nilihasmasika sana
Ila kiti nilichojifunza ni Kwamba Siku zote nitawaheshimu vijana wapiga Debe na Wamachinga, kwanza niseme tu kwamba wengi niliowahoji si tu kwamba walinihakikishia bali walinionesha kadi zao za Kupiga kura, Ni watu ambao kwao hawana cha kupoteza tofauti na sisi wafanayakazi wa Uma ambao hata kuinua Mkono wa Pipoz Power tunaogopa maana wale Nyoka wa TISS wako kila mahala
Hawa Vija ambao wengine wanawaita wahuni nawaheshimu sana na Historia daima itawakumbuka, Leo Mji Mzima wa mbeya Ulijaa Bendera za CHADEMA kwenye daladala, kwenye baiskeli na hata Pikipiki, ni vijana ambao wanaenjoy hii Game ya Siasa kuliko akina sisi Vitambi Mbele, wako huru kuonesha Hisia zao hata Mbele ya mkuu wa Mkoa
Kwa Hili nawashukuru sana CCM kwa kuwatelekeza hawa Vijana na sasa ndio watakaoikomboa hii Nchi
Dr. W Slaa ukiingia madarakani Jaribu kuwakumbuka hawa Vijana ambao CCM imekuwa ikiwarubuini miaka nenda Rudi! Uwatengenezee mfumo utakaowawezesha wale ambao wako tayari kurudi Darasani wafanye Hivyo
Nina mambo mengi sana ya Kuandika Juu ya Nilichokiona lakini muda sina
Ila kwa kifupi ni Kwamba Wana Mbeya hakika watahesabiwa katika mapambano haya