MSEZA MKULU
JF-Expert Member
- Jul 22, 2011
- 3,763
- 5,607
wasalaam ndugu. Mimi ni mwanachama msomaji na mfuatiliaji wa karibusana wa jukwaa hili kuliko majukwaa yote ktk forum hii ingawa sina muda mrefu sana . Sina uhakika kama wapenzi wenzagu wa jukwaa hili lenye kujenga huwa mna utaratibu wa kukutana nakubadilishana mawazo na mbinu za kujikwamua kimaisha, kama ndivyo naomba nipewe taarifa marafiki zangu. Kama hakuna mnaonaje tukatenga siku moja tunapoelekea mwisho wa mwaka kuwa pamoja na kubadilishana mawzo haya ikiwepo kujenga ukaribu zaidi maana wengi tunafaamiana kwa njia ya nicknames.
Ahsante nawasilisha.
mkuu kama uko Dar unaweza kuomba appointment na wenyeviti wa jukwaa hili via PM. Jamaa wanaitwa malila, LAT, Kanyagio, Maskini Jeuri, Newmzalendo etc. Naamini hawa jamaa watakupa mwanga kwenye uwekezaji, sababu inakuwa shida sana kukutanisha watu wengi kwa wakati mmoja.