Habari wadau,
Ishu ipo ivi.
Nina babu yangu ambae anamjengo wake alimkodisha mama mmoja.
Huyu mama amefungua skuli na amefanya ni kama orphanage house.
Sasa ikafika kipindi huyu mama akawa halipi kodi na hataki kutoka ndani ya nyumba. tukatumia busara ya kuwa basi aendeleze kulipa kodi ya mjengo. Lakini akawa anatupiga chenga. Sasa ikafika wakati familia ikasema enough is enough. Tukaamua kwenda mahakamani...
Mahakamani ikawa mzungusho mrefu tu wa miaka huku yule mama akiendelea kuishi kwenye hio nyumba. Mwisho tukampelekea Notice ya miezi mitatu, tukampa miezi mitatu free ajitaarishe kuhama. Basi akaja na option kuwa, tumuuzie yeye nyumba, kwa kina chake akataja kiasi fulani cha fedha, basi na sisi ili kuepusha malumbano, tukamkubalia atupe hizo pesa ili tumuachie nyumba. Lakini yalikuwa ni maneno matupu ili a delay kuhama. Tukaona anatuchezea, tukarudi mahakamani. Kwa bahati nzuri haki imechukua mkono wake. Mahakama ikaamuru mama ahame, tena "IMMEDIATELY' baada ya kupewa notice huko nyuma na kukataa kuhama, pia na alipe fine ya kiasi fulani. Sasa sisi tulivopata barua hio kutoka kwa Jaji tukenda kituo cha polisi. Kwa mujibu wa lawyer wetu, na kwa mujibu wa barua ya mahakama, manake tuna haki ya kwenda kumhamisha muda wowote.
Kwenda kituoni, mkuu wa kituo akatuomba hio Drawn Order tulopewa. tukampa aisome ili ajiridhishe. Mkuu huyu akajiridhisha na akatupatia askari wawili kuambatana nao.
Tukafika kwenye nyumba, msimamizi wa watoto ndani akajidai mama hayupo kampigia simu atakuja baada ya masaa mawili. Sisi tukakataa kuwa hatuwezi kukaa masaa mawili kumsubiri aje.
Kumbe yule mama alikuwepo ndani kajifungia, wale polisi wakatoa warning, ikawa msimamizi anakomea milango kwenye nyumba. Basi tukaamua kutumia force kuvunja mlango. Mama akatoka nje hafla, anasema hawez kutoka mana hakupokea notice. Tukamuonesha barua ya mahakama inayomhitaji aondoke haraka ndani ya nyumba na kuwa alishapewa notice huko nyuma akakataa kuhama. Mama akatupa chini akileta ubishi, askari wakatupa amri ya kutoa vitu.
Tukavitoa vitu nje tukawakusanyia. Mpaka vikamaliza.
Mara hafla akaja yule mkuu wa kituo, akatoa amri vitu virudishwe ndani. Ukaanza mzozo, akatoa mikwala na kusema tupigwe mabomu (tear gas) ikawa mzozo mkubwa. mwisho tukatulizana.
Huyu mama kumbe alitoka akenda kwa mkuu wa kituo, hatujui nini kimezungumzwa uko.
Sasa mimi nashangaa, mkuu huyu huyu amesoma barua na akajiridhisha, na akatupa askari yeye mwenyewe tuambatane nao kuhakikisha usalama, kisha sasa ivi anatugeukia. Tulipomuuliza akatwambia kuwa wao kituoni hawakupokea barua kutoka mahakamani wasimamie zoezi. Ndio ulikuwa utetezi wake. Lakini barua hio inatupa right ya sisi kama wamiliki kwenda kumtoa huyo mama na yeye mkuu wa kituo wakati alipokuja tena amekiri kama kweli.Lakini Mkuu huyu kwa ukali akasema zoezi lisitishwe.
Sasa naomba kuwauliza wanajamvi. Mkuu huyu wa kituo kafanya sawa kutuzuia sisi kutekeleza amri tulopewa na Mahakama? Ikiwa hayupo sawa je sheria zinasemaje kuhusu huyu mkuu wa kituo?
Kwa kweli kanichafua sana, tumetoa vitu vyote nje halafu anatwambia turudishe vitu ndani? (Walirudisha wenyewe)
Ushauri na msaada wa kisheria please wanajukwaa
Nataka kupambana na mkuu wa kituo kwa kutuzia kutekeleza amri ya Mahakama.
Asante