Mkuu wa Mkoa Dar wapige chini baadhi ya Viongozi wa mashirika Soko la Kariakoo

Mkuu wa Mkoa Dar wapige chini baadhi ya Viongozi wa mashirika Soko la Kariakoo

Pdidy

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
57,951
Reaction score
32,619
Gazeti za jana zimesikitisha sana kwa yanayoendelea pale Kariakoo.

RC wangu, wakati doll ikikagua yale majina, nikujuze tu kuwa mamlaka yako inaruhusiwa kuwaondoa viongozi wa Shirika la Masoko Kariakoo mapema.

Kumekuwa na kama dili za ajabu, soko likiungua viongozi wanafikiri ndio sehemu ya kupigia hela hapo.

Sio mara ya kwanza ninasema hivi, hata lilipotokea huko nyuma majina yalidukuliwa upya.

Sasa na round hii, walewale, sura zilezile tena wanataka kufanya watu wajinga na kutajirika wakati watu waliopoteza mali zao, waliokuwa maskini ghafla.

Hapana, hata baada ya kupitia upya, ombi langu ni kuwa ili iwe fundisho kwa wengine watakaounguliwa masoko na kutaka kufanya sehemu ya kuneemeka kupitia waathiriwa, waondolewe Mheshimiwa RC, waondolewe na TAKUKURU ikague moja baada ya lingine.

Hao watu wamekuwa wakilipa kodi na risiti zao, leo hii wanatokea viongozi ati tunatambua 891 tu. Hao wengine walikuwa wanauza makanisa? Inaumiza sana. Anyway, shukrani kwa kulitatu vyema.

Ninaamini suluhisho likipatikana, hao viongozi wapitishwe na wapangiwe kazi zingine.
 
Hakuna atakayebadilishwa wale wamewekwa pale na wakubwa siasa tu inaendelea. Nimewahi kuona ubabe na rushwa inayofanywa na viongozi wamachinga kariakoo nikagundua kitu
 
Kariakoo ni zaidi ya uijuavyo, mmachinga mwenye meza barabarani au mbele ya duka la mtu analipa kodi zaidi ya laki kwa mwezi na serikali ipo haifanyi lolote na wala haipati chochote
 
Hakuna atakayebadilishwa wale wamewekwa pale na wakubwa siasa tu inaendelea. Nimewahi kuona ubabe na rushwa inayofanywa na viongozi wamachinga kariakoo nikagundua kitu
Uligundua kitu gani mkuu
 
Back
Top Bottom