Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Mkuu wa Mkoa wa kusini Unguja Visiwani Zanzibar, Ayoub Mohammed Mahamoud, ametangaza uamuzi mpya wa kuwapatia Wafanyakazi wa Ofisi yake chai ya asubuhi ikiwa na kitafunwa cha mikate wenye siagi kuanzia kesho Jumatatu May 6 2024 ili kupunguza Wafanyakazi kuzurura saa za kazi, kuongea na simu mara kwa mara pamoja na kutoka nje kwenda kununua urojo.
RC Ayoubu ameyasema hayo leo wakati akifungua kampeni ya ‘amshaamsha Kusini’ ikiwa ni mahususi kwa Watumishi wa Serikali lengo likiwa ni kutokomeza uchelewaji makazini, kuzurura muda wa kazi na matumizi ya simu vitu ambavyo amesema haridhishwi navyo kwani vinachelewesha maendeleo ya Wananchi ambapo amesisitiza kuwa gharama zote za chai na vitafunwa zitakuwa zikitoka kwenye mshahara wake yeye Mkuu wa Mkoa.
#Tanzania2025