Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Wakuu,
Hivi mna uhakika hawa viongozi wanaoteuliwa na Rais huwa wanafanyiwa vetting kweli kabla ya kupewa vyeo?
Wakati nazunguka leo mtandaoni nimekutana na clip ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Kenani Kihongosi ambaye ni kama alikuwa anatishia wananchi kushiriki katika zoezi la kulinda kura.
Kihongosi amewataka wananchi wa Simiyu kurejea nyumbani mara tu baada ya kupiga kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024.
Soma pia: Chalamila aliagiza Jeshi La Polisi kuwashughulikia wananchi watakaopinga matokeo ya Uchaguzi ujao wa Serikali Za Mitaa
Amesema kuwa jukumu la kulinda kura ni la mamlaka husika, hivyo wapiga kura wanapaswa kumaliza zoezi hilo na kurudi majumbani mwao.
"Na ukishapiga kura rudi nyumbani. Kuna watu wanawaambia watu wanaenda kulinda kura. Na sisi tunasubiri hao walinzi wa kura watuambie hiyo kazi wamepewa na nani. We piga kura kalale. Suala la Uchaguzi achia mamlaka za uchaguzi."
Source: Global TV Online