Mkuu wa Mkoa Tabora awahakikishia usalama washiriki wa UMISETA 2024

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Matiko Chacha amewahakikishia Usalama wanamichezo na wageni waliopo Tabora kwa ajili ya kushiriki Mashindano ya UMISETA 2024.

Ameeleza hayo leo tarehe 18 Juni 2024, wakati akizungumza kwenye Mashindano hayo ya Umoja wa Shule za Sekondari Tanzania, yanayofanyika Mkoani Tabora kwa mara ya tatu mfulululizo.
"Tuna Wanamichezo zaidi ya Elfu tatu na waalimu zaidi ya mia saba, hii ni idadi kubwa lakini hadi kufikia sasa wote wapo salama na mkoa kwa ujumla uko salama," amesisitiza RC Chacha.

Kuhusu maazimio ambayo yametolewa na viongozi mbalimbali juu ya kukuza michezo, amesema kuwa Mkoa utayasimamia yote yaliyoazimiwa kwa ajili ya maendeleo ya michezo nchini.

Akitoa salam za Mkoa kwa Mgeni rasmi Waziri wa Sanaa Utamaduni na Michezo Dkt. Damas Ndumbaro, Mkuu huyo wa Mkoa amemhakikishia kuwa wamejipanga kahakikisha kuwa michezo inapewa kipaumbele katika shule mbalimbali.

"Viongozi wetu wa kitaifa akiwepo Waziri Mkuu wakati wa uzinduzi rasmi wa mashindano ya UMITASHUMTA & UMISSETA 2024 alisisitiza juu ya kukuza na kuendeleza vipaji vitakavyoibuliwa katika mashindano haya, na sisi kama mkoa tumejipanga kutekeleza hilo," amesema Mkuu wa Mkoa wa Tabora.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…