The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Paul Chacha ametoa siku moja kwa Kaimu Mkurugenzi wa Halmshauri ya Manispaa ya Tabora Dkt. Shani Mdamu ahakikishe kukamatwa kwa mkandarasi anayetekeleza mradi wa ujenzi wa majengo Kituo cha Afya cha Itetemia kilichopo Manispaa ya Tabora kutokana na tuhuma za kutowalipa fedha vibarua ambao anashirikiana nao katika ujenzi wa majengo hayo ilihali alishalipwa fedha zote za utekelezaji wa mradi huo.
RC Chacha ametoa agizo hilo wakati alipofika kwenye kituo hicho cha afya kwa ajili ya ukaguzi wa ujenzi wa majengo hayo ikiwa ni mwendelezo wa ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo mkoani humo.
Kwa mujibu wa vibarua hao, wamekuwa wakifanya kazi ya ujenzi wa majengo hayo kwa muda mrefu lakini mkandarasi huyo amekuwa akiwapiga danadana kuwalipa fedha zao kwa muda wa mwaka mmoja sasa.
Pamoja na mambo mengine RC Chacha ameridhishwa na hatua za ujenzi wa Shule ya Sekondari Ihumbi iliyopo wilaya ya Nzega mkoani Tabora na kuwasihi wananchi kuwapeleka watoto wao katika shule hiyo ambayo ujenzi wake umekamilika.