Wazungu na sera za brainwashed wametuweza Sana Africa tukasahau vya kwetu tukafuata ya kwao
Leo usipo mpa pesa mwana mke humpend usipo mbusu humpendi,akiona kitu kwa mwenzie akikuomba usipo mpa humpend yote haya brainwashed
Leo chalamila kuwatia stik vijana imekuwa gumzo Sana mitaan yeye Ni mzazi pia
Mbona enz zetu usipompokea mzee mzgo wake au kumsalimia au kutukana tulipata stick za kutosha na akienda kusema kwenu ding lao ana wew Tena
"Tulipotoka na tulipo siko na kurud tulipo toka tumeshachelewa"
Wacha tupangiwe na weupe maisha yao yawe yetu
Hamna cha wazungu wala nini, Waafrika tumekua na huu ujinga sana wa kulaumu wazungu kwa kila upumbavu wetu, hata hizo enzi za mababu zetu mwanamke asingekupenda kama wewe mzembe usiyeleta chochote nyumbani, ndivyo mwanamke ameumbwa tangu enzi za mitume.
Vijana wazembe mnataka mvae mlegezo na kulala kwenye kochi kila siku kisha mpendwe na wanawake, tia bidii, tengenza hela, hakuna mwanamke asiyependa stability, ukimwoa akuzalie watoto atahitaji wahakikishiwe vitu vya msingi kama elimu, chakula, mavazi, nyumba n.k.
Halafu hili la kuwapiga watoto siliungi mkono, haswa kama hawa waliofikisha umri wa kubaelehe, mimi hapa ni mzazi na nawalea wanangu bila kipodo, na wako poa tu hamna mibangi bangi wala vituko, tunaendana freshi, pakiwa na matatizo tunawekana sawa. Sio kwamba naiga wazungu, ni maamuzi yangu ya vipi nitaendesha familia yangu.
Ukifuata sana watemi au bullies shuleni, hao ambao hutia mashule viberiti utakuta wamekua abused somehow na wazazi wao, kwamba tangu akiwa mdogo amekua akitembezwa kichapo mpaka hapo alipo. Tazama hiyo video uone kama kuna chochote huyo mkuu wa mkoa anakifanya, yaani anawacharaza ila hata hawatikisiki, wamezoea na wanaona kama anawatekenya vile.