Hii sio fursa hata kidogo, World Bank walitoa report inayoitwa doing business roadmap na Tanzania ilitajwa kama nchi 121 kwa kuwa na mazingira ya kufanya biashara. Toka wakati huo mapambano yalielekezwa katika atleast tukitajwa tena basi tusizidi 2 digits, yaani tutoke kule kwa 120 tufikie angalau 90.
Ukweli mazingira ya kufanya biashara Tanzania ni magumu mno na anyesababisha ni serikali, taasisi zake na nyie wananchi wenye uwelewa duni. Si lazima serikali ipate katika kila biashara wakati mwingine iangalie manufaa wanayopata wananchi wake. Ukiangalia stand mpya utaona kabisa aliyebuni hakushirikisha wafanya biashara wala abiria yeye alikaa na wahafidhina warasimu wakapenda jengo.
Wafanyabishara wanashindana katika huduma wanazowapa abiria wao sasa ukilazimisha waende sehemu kuingia unalipia, choo unalipia na hakuna value yeyote anayepata abiria zaidi ya kero kwa wapiga debe. Waliotoa pesa zao wanatafuta wateja ili kurudisha mitaji yao na kupata faida. Tozo na ushuru ni mambo yanayofanya mazingira ya biashara kuwa magumu zaidi, mwambie mkuu wa mkoa aone huduma wanazopata watu wake na multiplier effects zaidi kuliko tozo ambazo ni kero zaidi kuliko kuleta faida. Serikali ipo kuhudumia watu wake wanaolipa kodi.
""Ukiwa na stendi binafsi kumi, una karibu milioni 100 kwa mwaka" haya ndio mawazo yenu yanayofanya nchi hii isiendelee. Ebu angalia kiasi gani cha kodi wamelipa, ajira walizopata watu wenu, diesel waliyonunua na kodi ulizokata huko.