Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh. Rosemary Senyamule Amewaomba Wakazi wa Dodoma na Wananchi Wote Kwa Ujumla Kufika Mapema Katika Maadhimisho ya Kuzaliwa Kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Yatakayo Fanyika Katika Uwanja wa Jamhuri Dodoma Tarehe 05 Februari 2025.
“Hapa ningependa kutumia nafasi hii kuwatangazia Wakazi wa Dodoma wanaoweza kupika uji mzuri wa aina yoyote ile, uwe ni uji wa muhogo, uji wa ulezi, uji wa mchele, N.K. Wafike hapa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa(Mkapa House) waonane na Afisa Biashara wajisajili, siku ya tarehe 05.02.2025 watatoa huduma ya kuwagawia uji Wananchi watakaokuwepo Uwanjani kwa utaratibu watakaolekezwa, na watalipwa pesa yao hapo hapo kulingana na kiasi cha uji watakachokuwa wamepangiwa kuleta.”