#COVID19 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya amesema Chanjo itakwenda nyumba kwa nyumba

ana matingo fijo ,huyu rc analazmisha watu kuchanjwa!!!
 
Sasa kama una ujuzi kwann hamtoi huduma mna waachia wanasiasa walete ujinga kwenyr taaluma yenu?
Kaka kazi ya chanjo si siri. Vijidudu vya ugonjwa vilivyodhoofishwa vinaingizwa mwilini, mfumo wa kinga wa mwili unavitambua na kuandaa seli za kuviua. Wakati vijidudu vya ugonjwa vinafika, seli za kinga zinaviua. Mfumo asilia wa kinga kwa kawaida unafanya kazi hiyo peke yake, lakini unahitaji muda. Kama ugonjwa mpya (kama Covid 19) unatokea, mashambulio ya ugonjwa yanaweza kuleta hasara haraka kabla mfumo wa kinga umejifunza, basi mtu atakuwa mgonjwa sana hadi kufa. Mfumo wa kinga ni mdhaifu zaidi kwa wazee na watu wenye magonjwa kama usukari, kansa na kadhalika, hapo sababu watu hao wanakufa zaidi kuliko vijana, au watoto.
Chanjo zote, pia zile za Covid19, zina kazi ya kuuamsha mfumo wa kinga wako na kuuandaa kwa shambulio lijalo.
Kuhusu Israeli umesikiasikia tu kitu mahali fulani, na unaisambaza bila kukichungulia.
Ninakuambia si kweli!
Ukitaka kunipinga, lete chanzo. Kama huna cha kuonyesha, heri usisambaze habari za uwongo
Tafadhali!!
Chanjo za Covid zinafanya kazi na zimethibitishwa katika nchi nyingi kuwa zinakinga. Si asilimia 100, lakini kwa watu wengi sana sana!
 
Hivi ni upi utofauti wa ubora kati ya chanjo moja hadi nyengine, yani kipi kinaangaliwa ili kuweza kujua kuwa chanjo fulani bora zaidi kuliko chanjo nyengine?
 
Ila kwa taarifa zilizo chini ya kapeti kuna amri inakuja kutolewa punde kwa kila mtoa huduma ama muuzaji anatakiwa awe amechanjwa.
Baadae watakuja katika majumuiko ya dini na masoko makubwa.
Time will tell
Ataaibika huyu mama ajaribu.
Alishaagiza watu wavae barakoa wananchi ... hawavai isipokuwa yeye na msafara wake.
Aliagiza chanjo... hawajachanjwa hata wan CCM wenyewe.
Ajaribu aone.
 
Heeeee siijui kala maharage ya wapi? Hawa viongozi wa hv ndo anawakataa king msukuma.ameshindwa kubuni mambo ya maana yenye maslahi kwa nchi,analipuka na lake tuuu.
 
Usimsumbue jamaa angalia statistics hiyo hapo pia nenda google uangalie uone israel wanataka kuwacjoma wananchi wao dozi ya 4 na booster kwa sababu chanjo hazijawasaidia.
Ishu ni kwamba wenye elimu hawawezi tumia ubongo wanasubiri billi gates na wazungu wataawaambia nini cha kukariri.
F*ck off

 
ajarbu kija na vichanjo vyake labda achanje mbuzii
 
Nilijua huyu jamaa intelligent kumbe nilikuwa wrong.Anyway,kazi njema.
 
Kaka unachekesha! Napenda watu wanaoandika "F*ck off" na wakati huohuo kujitambulisha "JESUS CHRIST THE SON OF GOD IS MY LORD". Tutumaini Lord wako asisome Jamiiforums?

Basi kuhusu takwimu narudia: Huelewi unachonakili. Ukipenda kuargue bila matusi, basi tuangalie takwimu ya Israel tangu mwanzo hadi sasa bila kukatakata vipande vidogo (maelezo kwa rangi kibichi niliongeza kwa manufaa yako):

Tunaona kwamba chanjo pamoja na masharti ya kukaa mbali / kuvaa barakoa yalisaidia kupunza vifo kabisa. Pale Israeli wana asilimia 17 wanaokataa chanjo (hasa kwa sababu ya kidini - wana waGwajima wao..).
Tangu mwisho wa masharti hao 17% walifaulu kusambaza wingu jipya kwa wengine.
Naongeza picha nyingine kutoka gazeti la Haartez (Israel's unvaccinated 17% now account for nearly half of COVID deaths)

Inaonyesha: Ndiyo, kuna maambukizi kadhaa pia kati ya watu waliochanja. Picha ya pili kutoka Haaretz inaonyesha namba halisi; unaweza kuona (unaweza, je?) kwamba kutoka idadi kubwa sana ya vifo imetokea kutoka hao milioni 1.6 ambao hawakuchanja (mstari mwekundu), vifo vingine kutoka hao milioni 8.5 waliochanja.
Ni vema kukumbuka tofauti kubwa kati ya nchi kama Israeli na tanzania ni muundo wa wakazi kiumri. Maana zaidi ya asilimia 90 ya vifo inatokea kati ya watu wenye umri juu ya miaka 60; watoto na vijana chini ya miaka 25 hivi asilimia ya vifo ni kati ya %% 0-1.
Ona tofauti ya muundo huo kwa namba:

Hapo tunapata sababu ya kuwa na vifo vichache kiasi Tanzania, hata hivyo kati ya wenye umri mkubwa sijaona tofauti kimsingi. Maana vijana wanambukizwa pia, lakini katika umri huo kwa kawaida mfumo wa kinga (immune system) unatosha kuzuia ugonjwa mkali wa Covid.
Ila hata vijana wanaweza kuambukiza wengine wenye umri mkubwa. Kwa hiyo: ukimpenda baba na mama mzee au bibi na baba - jaribu kujipatia chanjo!!! Angalau utumie tahadhari!

Halafu nchini Sweden (takriban idadi sawa ya watu kama Israel) masharti bado yapo kwenye mwezi wa Septemba 2021, pamoja na chanjo. Tuone jinsi namba zao zitabadilika watakapofuta masharti mwezi wa Oktoba!
 
Hiyo nisawa kabisa
 
Wasuburi majambia, tumechoka na ujinga wao.
 
Hivi watu km hawa huwa wanaokotwa wapi? Khaaaah [emoji23][emoji23][emoji23]
Ila Mbeya wana tabu San, kila RC wao lazima awe na mapungufu mweeeeh.
 
Aanzie nyumbani kwake yeye na mke wake na watoto wake wote!! Inabidi afundishwe nini maana ya hiari!! Aachie ngazi! Hatoshi kwenye kiti chake!! Hana nguvu ya ushawishi badala yake anataka kutumia nguvu kinyume na maelekezo ya mkuu wa nchi, huo ni UASI!!! Mkuu huyo wa mkoa ajue kuwa anafanya UASI kwa kukiuka maelekezo ya RAIS kuwa chanjo ni hiari!! AJIUZURU!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…