Lazia Sultan
Senior Member
- Jun 4, 2020
- 120
- 328
Tarehe 5 September 2020 ndugu Gelasius Byakanwa aliwaita watumishi wanaofanyia kazi kwenye taasisi zinazomilikiwa na watawa wa shirika la kikatoliki la Mt. Benedicto Ndanda kwenye kikao kifupi Cha kuzungumza nao.
Watawa hawa wana watumishi wengi kwani ndiyo wanaomiliki Ndanda Refferal Hospital, Abbey sec School, Abbey pure drinking water, printing press and bookshop, nursing school, trade school na workshop nyingi Kama plumbing, welding, garage, carpentry na takataka nyingine nyingi.
Hivyo watawa hawa wameajiri watu wengi sana ambao mh mkuu wa Mkoa amecheza karata zake kwenda kuwaombea kura wagombea wa CCM katika uchaguzi mkuu hapo October 28 mwaka huu.
Mmoja wa waliohudhuria kanambia walipewa taarifa ya kikao hicho cha mkuu wa Mkoa ila hawakujua agenda ni nini, walizikuta huko huko, ambazo kwa asilimia kubwa ni kuwataka washiriki uchaguzi mkuu kwa kuwachagua ccm kwani wamekuwa bega kwa bega na taasisi hiyo tangu zamani, hivyo waendeleze mshikamano huo.
Kwa mtazamo wangu sasa naanza kuona jinsi CCM walivyopoteza matumaini kutoka kwa watumishi wa umma hadi kuamua kucheza karata zao kwa private sectors. Wameanza kuukimbia na kuuogopa mzimu wao wenyewe hadi wanaenda kwa jirani.