Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Soma, Pia:
+ Vurugu kali zimezuka Uwanja wa CCM Kirumba wakati Simba SC ikifanya mazoezi kuelekea mechi na Pamba Jiji hapo kesho
+ Simba yalaani matumizi ya Polisi kuwazuia kufanya mazoezi katika uwanja wa CCM Kirumba kuelekea mchezo wa dhidi ya Pamba
Kupitia Crown FM, Said Mtanda, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza amesema:
"Mimi ninaamini mpira utachezwa leo, na mkuu wa mkoa akitembelea sehemu ya mkoa wake iwe uwanjani au amekwenda hospitali haina maana kwamba ameenda kuwahujumu wagonjwa au wachezaji"
"Mimi nikiwa ofisini kwangu jana nilipata taarifa kuna dalili za uvunjifu wa amani, baadhi ya makomandoo wa Simba Sc wamewahold viongozi wa Pamba Jiji Fc ambao walikuwa uwanjani wakifanya mazoezi kabla ya kuondoka, sasa wamefunga milango yote, wale vijana walipoona watashambuliwa wakaenda juu VIP wakafunga milango...."
"Makomandoo wa Simba sc wakaanza kuvunja vioo vya VIP ya CCM Kirumba, lakini baadae wakaanza kuvunja milango, kwa hiyo wakanipigia mimi, nikampigia Mkurugenzi wa jiji, lakini nikawapigia jeshi la polisi, na nikafikiri ni busara kusogea eneo hilo ili baadae mambo yasije kutangazwa ambayo sio sahihi.... lakini pia kuhakikisha jeshi la polisi linafanya kazi yake kwa weledi"
"Sikuingia uwanjani na wala sikuwa na nia ya kuona mazoezi ya Simba Sc, kwa sababu mimi ndio mgeni rasmi, nina haraka gani ya kuwaona Simba Sc wakati leo nilikuwa na uwezo wa kuiona Simba Sc kwa utulivu kwa dakika 90?"