Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, ameongoza kikao muhimu na wamiliki wa hoteli mkoni humo

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, ameongoza kikao muhimu na wamiliki wa hoteli mkoni humo

Venus Star

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2018
Posts
26,519
Reaction score
78,311
Septemba 22, 2024, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Ahmed Abbas Ahmed, aliongoza kikao muhimu na wamiliki wa hoteli mkoani Ruvuma. Kikao hiki kilifanyika kama sehemu ya maandalizi ya kuimarisha sekta ya utalii, hasa wakati huu ambapo mkoa unasherehekea Tamasha la Tatu la Kimataifa la Utamaduni, lililoanza rasmi tarehe 20 Septemba na litaendelea hadi 23 Septemba 2024.

DSC_3057.jpg


Katika kikao hicho, Kanali Ahmed aliwapongeza wamiliki wa hoteli kwa juhudi zao za kuimarisha huduma za malazi, akisisitiza kuwa sekta ya hoteli ina mchango mkubwa katika ustawi wa utalii mkoani. Pia, aliwataka wamiliki wa hoteli kuzingatia ubora wa huduma na kuhakikisha kuwa wageni wanaopokea wanapata uzoefu mzuri na wa kipekee.
DSC_3092.jpg


Katika kikao hicho, Mkuu wa Mkoa alitoa wito kwa wamiliki wa hoteli kutoa huduma bora zaidi wakati wa tamasha hili. Aliwataka kujipanga ipasavyo kwa kuhakikisha kuwa wanaleta vivutio zaidi kwa watalii, kama vile mapishi ya asili na huduma za ziada zinazohusiana na utamaduni wa eneo hilo.

DSC_3042.jpg


Kwa upande wao, wamiliki wa hoteli walieleza kuwa wamejipanga vyema kuhudumia wageni, huku wakihakikisha wanakidhi mahitaji ya kimataifa. Wengi walisema wameboresha miundombinu na huduma zao kwa kiwango cha kuridhisha, ili kuwa tayari kwa ongezeko la wageni linalotokana na tamasha hilo.
 
Kuna mtu picha ya kwanza anafanana na Cpt. Komba, je ni nduguye?
 
Back
Top Bottom