Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma azindua tamasha la majimaji selebuka 2022

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma azindua tamasha la majimaji selebuka 2022

RAHA KAMILI

JF-Expert Member
Joined
Dec 5, 2014
Posts
203
Reaction score
83
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mh Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge, ameagiza ushiriki wa wilaya na halmashauri zote za Mkoa Wa Ruvuma kwenye tamasha la Majimaji Selebuka litakalofanyika kuanzia tarehe 23 hadi 30 July 2022 mjini Songea. Tamasha hili limekua jukwaa kuu la biashara, kutangaza utalii, kuchochea vipaji, utamaduni , mashindano ya debate kwa shule na michezo, hivyo linatoa fursa adimu kwa mkoa wetu wa Ruvuma.

Pia mwaka huu tamasha hili litakuwa na mashindano ya baiskeli ya km 165 toka Songea hadi Mbamba bay, mbio na mpira wa miguu na kikapu. Ili kuwapa urahisi washiriki kwenye Majimaji Selebuka imezindua tovuti yenye zaidi ya hoteli 200 kwa ajili wageni.

Pamoja na kutangaza vivutio vya utalii vya mkoa wa Ruvuma, Majimaji Selebuka inachochea biashara, elimu, sanaa, michezo kwenye ukanda wa kusini

Majimaji Selebuka ni tukio linalofanyika kila mwaka Songea, Ruvuma ambapo mwaka huu litazizima kuanzia tarehe 23 hadi 30 Julai. Kujisajili ingia majimajiselebuka.co.tz


 
Mbona hatangazi kama kuna samaki aina ya mbufu ambae huliwa na ugali wa muhogo, mbona hasemi mberere kua wapo, lakini pia dagaa Nyasa wanaopatikana malawi na mbambabay, manda huko aeleze wanasoko pia Congo
 
Matamasha daily
Wabongo we waweke wasani
Sjui nandy konde kiba,singeli
Shida zote wanasahu

Ova
 
Watani zangu Wangoni hapo watangonoka hadi kukuche
 
Back
Top Bottom