Wakati taifa linaeleka kenye Uchaguzi, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha amewaomba wanasiasa wasitumie fursa ya kuwafuturisha wananchi kama rushwa ya kwenye uchaguzi
"Niwaombe sana viongozi wa kisiasa wasitumie visivyo mwezi huu. Tunajua kuna kuandaa futari kwa waumini wa dini zetu zote hususani kwa kweli lazima tukiri futari inayohusu waumini wa dini ya kiislamu ambayo mara nyingi ndio huonekana dhahiri kabisa.
Niwaombe viongozi wa kisiasa kama kweli wana imani ya kuandaa futari, waandae futari kwa ajili ya kukidhi imani za waumini wetu wawe wa kikristo wawe wa kislamu lakini ningewaomba wasiandae futari ili futari hizo wapitishe ushawishi wao wa kisiasa kwa sababu mifungo hii lengo lake sio hilo"
"Na sisi tunawaomba wasiandae futari zenye asili ya rushwa kawa ajili ya uchaguzi"