Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida, ACP Amon Kakwale, amewataka waandishi wa habari kutumia kalamu zao kama nyenzo ya kuimarisha mshikamano wa Watanzania badala ya kuleta mgawanyiko.
Akizungumza katika mkutano mkuu wa mwaka wa waandishi wa habari mkoani Singida, Kamanda Kakwale alisisitiza umuhimu wa waandishi kuandika taarifa zenye uwiano na zisizoegemea upande wowote ili kutoa taswira chanya kwa jamii.
Soma pia: Msemaji Mkuu Wa Serikali: Serikali haifurahishwi na taarifa potofu katika kipindi hiki cha Uchaguzi. Watanzania fuateni sheria
Katika kipindi hiki cha maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa, Kamanda Kakwale aliwahimiza waandishi na wananchi kwa ujumla kudumisha umoja na kutambua kuwa maisha yanaendelea hata baada ya uchaguzi.
Mkutano huo uliandaliwa na Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Singida (SINGPRESS) kwa lengo la kujadili changamoto, maadili ya kazi, na mahusiano na wadau wa habari, huku pia ukitilia mkazo mshikamano kati ya waandishi wa habari wenyewe.
Source: AFM Radio