Mkuu wa Polisi Songwe: Hakuna kupiga fataki katika sikukuu za mwisho wa mwaka bila kibali

Mkuu wa Polisi Songwe: Hakuna kupiga fataki katika sikukuu za mwisho wa mwaka bila kibali

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wakuu,

Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe limepiga marufuku wananchi kulipua vilipuzi (fataki) bila kuwa na kibali cha Jeshi la Polisi katika Sikukuu Za Krismasi na Mwaka Mpya.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe Kamshina Mwandamizi Msaidizi wa Polisi Augustino Senga amesema Jeshi la Polisi limejikita katika kuhakikisha ulinzi na usalama unakuwepo muda wote na maeneo katika Mkoa wa Songwe hasa kipindi hili cha sherehe za Mwisho wa Mwaka.

Aidha Kamanda Senga amewataka watumiaji wa vyombo vya moto Nà watumiaji wa barabara kuhakikisha wanazingatia Sheria na taratibu za barabarani ili kuepusha ajali na madhara mengine barabarani.




Source: Wasafi FM
 
Ushamba huo. Lazima nikaone mabomu Dynasty.
 
Haiishi mpaka iishe,,

Wawezaje kuzuia watu kusherehekea ili hali ndo sikuu ya kufunga mwaka wa kufosi🫵😂😂😂
 
Hapa arusha mt meru Hotel wanapiga za kibabe sana kila mwaka tunaendaga kuenjoy milipuko
 
Back
Top Bottom