Natambua watendaji serikalini mna mambo mengi yakushughulika ikiwa ni pamoja na kuhakiki utoaji wa elimu katika mazingira salama na bora. Pamoja hilo, wazazi ni wadau wa muhimu katika ufanisi wa utoaji wa elimu nchini na wajibu wao katika kuchangia huduma hizo inapostahili.
Hata hivyo, mkuu wa shule ya sekondari ya Chilonwa iliyopo Dodoma amekuwa akiburuza walimu na wazazi katika kutoa maamuzi ya uendeshaji wa shule hiyo.
Mfano;
i) mwaka jana aliagiza na kuwarudisha wanafunzi wa shule hiyo majumbani kwao kufuata mchango wa shilingi 10000 ya kufanikisha mahafali ya kidato cha nne ya 2014. Mchango huo haukuwa kwenye makubaliano ama mawasiliano na wazazi/walezi katika kuchangia.
ii) Shule hiyo pia inaendeshwa kwa wazazi ama walezi kuchangia mchele (32 Kgs), unga (32 kgs), maharagwe, sukari, chumvi, hela ya mlinzi, hosteli (100000). Pamoja na uchangiaji huo, taarifa za uhakika ni kuwa mchele huo hugawiwa kwa walimu na wanafunzi kula ugali tu kwa muda wote wawapo shuleni. Kibaya zaidi ni kuwa pamoja na idadi hiyo kubwa ya michango, wanafunzi huharakishwa kufunga shule kwa maelezo kuwa chakula kimeisha.
iii) Wiki hii ya 18/3/2015, mkuu huyo kawaambia wanafunzi wa kidato cha nne kuwa hawatafunga shule na wataanza masomo ya ziada kkuanzia jumatatu ya 23/3 kwakuwataka wachangie tena kilo 8 za unga, kilo 3 za maharagwe, na 2000 za matumizi mengine.
Swali kwa viongozi wa elimu toka TAMISEMI, wakaguzi na wizara ya elimu makao makuu kuwa ndivyo sekondari za umma zinavyoendeshwa? Ama hii ndio decentralization yenyewe?
Vinginevyo tusaidieni katika adha ya uongozi wa mkuu wa shule hii maana pia nasikia hutamba yenye ni kada wa CCM wa muhimu hivyo walimu na hata wazazi hawamtishi