Mkuu wa Shule Chilonwa afuatiliwe

Kilalo

Member
Joined
Apr 29, 2013
Posts
65
Reaction score
12
Natambua watendaji serikalini mna mambo mengi yakushughulika ikiwa ni pamoja na kuhakiki utoaji wa elimu katika mazingira salama na bora. Pamoja hilo, wazazi ni wadau wa muhimu katika ufanisi wa utoaji wa elimu nchini na wajibu wao katika kuchangia huduma hizo inapostahili.

Hata hivyo, mkuu wa shule ya sekondari ya Chilonwa iliyopo Dodoma amekuwa akiburuza walimu na wazazi katika kutoa maamuzi ya uendeshaji wa shule hiyo.

Mfano;

i) mwaka jana aliagiza na kuwarudisha wanafunzi wa shule hiyo majumbani kwao kufuata mchango wa shilingi 10000 ya kufanikisha mahafali ya kidato cha nne ya 2014. Mchango huo haukuwa kwenye makubaliano ama mawasiliano na wazazi/walezi katika kuchangia.

ii) Shule hiyo pia inaendeshwa kwa wazazi ama walezi kuchangia mchele (32 Kgs), unga (32 kgs), maharagwe, sukari, chumvi, hela ya mlinzi, hosteli (100000). Pamoja na uchangiaji huo, taarifa za uhakika ni kuwa mchele huo hugawiwa kwa walimu na wanafunzi kula ugali tu kwa muda wote wawapo shuleni. Kibaya zaidi ni kuwa pamoja na idadi hiyo kubwa ya michango, wanafunzi huharakishwa kufunga shule kwa maelezo kuwa chakula kimeisha.

iii) Wiki hii ya 18/3/2015, mkuu huyo kawaambia wanafunzi wa kidato cha nne kuwa hawatafunga shule na wataanza masomo ya ziada kkuanzia jumatatu ya 23/3 kwakuwataka wachangie tena kilo 8 za unga, kilo 3 za maharagwe, na 2000 za matumizi mengine.

Swali kwa viongozi wa elimu toka TAMISEMI, wakaguzi na wizara ya elimu makao makuu kuwa ndivyo sekondari za umma zinavyoendeshwa? Ama hii ndio decentralization yenyewe?

Vinginevyo tusaidieni katika adha ya uongozi wa mkuu wa shule hii maana pia nasikia hutamba yenye ni kada wa CCM wa muhimu hivyo walimu na hata wazazi hawamtishi
 
Sasa hapa ndio unajenga au unabomoa?!

Wazazi maskini tunapenda vya bure saaaana! Hatuoni matajiri wanavyojitoa kwa watoto wao alafu hao hao wanaojitoa utawasikia wakisema elimu ni bure.....tusipojitoa basi watoto wetu wataishia kuwa watumwa kila siku.
 

Umeelewa malalamiko ama tu ni kwa vile unaweza kusoma na kuandika lakini kutafsiri wakufanyie wengine?

Mkuu huyo wa shule anachangisha kilo 32 za mchele kwa kila mwanafunzi na vinalipwa na wazazi. wewe unakubali kuwa sahihi wanafunzi hao wasile wali hali mchele umechangwa na wao wenyewe?

Ni sahihi kuwarudisha nyumbani wanafunzi ili wakalete 10000 ya kufanikisha mahafali?
 
Mi naona mkuu yuko powa tu, hebu jaribu fuatilia vizur data zako,haiwezekan kg32 x total no.of students= kg? na hyo shule inawaalim wangapi?

watagawana magunia yote wataweka wapi? lakn hayo ni marupurupu ya mwl,tena kdogo cna,mnalalamika vimichango vidogo kama hvyo,wakat watu wanabeba mabilion ya escrow hawafanyw kitu,

kwa ushaur nchi hii sahz ukipata chance piga kisawa sawa,kama eneo ulilopo linaruhusu hata wazaz piga changa uso la maana cna tu,
 
tunaipeleka wapi Tanzania yetu ikiwa tumeweka mbele tamaa, uchu, wizi wa mali za uma, na dhuluma kwa tabaka la chini? Ee Mungu pigania wanyonge pande zote za dunia.
 
Mkuu kuhusu michango uelewa wangu ni kwamba bodi ya shule ndo huidhinisha hiyo michango...kwa maana hiyo mkuu wa shule hawezi kushirikiana na walimu katika hilo iulizwe bodi ya shule kama hiyo michango imeidhinishwa ....ila cha kufurahisha ni kuwa mkuu wa shule ndo huteua wajumbe wa bodi yashule!
 
Hayo ni baadh ya matokeo ya unaninyima ugal mi nakunyma mboga.

mwl mkuu sion kosa lake. huo ndo mtindo au style ya uongoz wa sisiem na seri kal yke.

tuamke tuamke tuamke, sababu tunao umia ni sisi wa third class..

sector ya walimu haithaminiw kabisa hasa serikalin ndo mana mtaan unamgundua mwl wa serikal na private wako tofaut kabisa ukiachalia wale wa zamani.

yaan mpaka sion umuhmu wa et utawaskia TUMEFUTA ADA HAYA SASA 32Kg zita tuhusu sana wazazi kwa hawa wa matishet kofia na kanga moja.
 
Hahahahahahaha ivi kuna tatizo gan kama mkuu wa shule atawaambia watoto wke wasifunge shule warud kusoma je angexema warud kwa ajil yakumlimia shamba c ingekua tabu zaid Alafu kingne ebu 2jaribu kufikiria pia tatzo ni elf 2000 na unga kilo 8 au kuna kngne ndg ye2 mtoa mada.
 
mkuu yupo sawa wagogo tumezoea kuombaomba tukiambiwa tuchangie maneno tushazoea vya bure ndo maana tunalalamika mkuu saf
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…