Mkuu wa Shule na Mzazi wa Mwanafunzi walinitengenezea zengwe hadi nikafukuzwa kazi

Hakuna kesi ya kufukuzwa kazi kwa ushahidi wa kufikirika na mwepesi kama huo hata kama ni kweli ulimtongoza huyo binti. Labda kama ungekuwa umemtafuna kweli, na ukakamatwa na vielelezo/vidhibiti vya kutosha! Mfano ujumbe mfupi kwenye simu, umekutwa naye ndani ya chumba chako na huyo mwanafunzi, umempa ujauzito, nk.

Wewe endelea kupigania haki yako. Ikiwezekana nenda kwa DAS, RAS, nk kutoa malalamiko yako. Na baada ya hapo fanya utaratibu wa kuomba kuhamia shule iliyo kwenye Kata/Tarafa nyingine ndani ya hiyo Halmashauri yako ili kuepukana na hizo changamoto.
 
Akiroga anamaliza mchezo wote tena bila wasiwasi
 
Mkuu wa shule ni kiongozi viongozi hawaangushani mkuu

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Ukweli unajua mwenyewe ila naamini haijasema kweli toka kwenye moyo wako.

Ukisema kweli nitakusaidia.
Kazi ni kwako kusema kweli au kuendelea kuongopa huku ukiwa jobless.
 
Kama una uhakika hukuwahi kuwa na matamanio ya kimapenzi na siyo tabia yako kuwatongoza wanafunzi,weka wakili.

Hiyo kesi ni ya kutungwa.
Vp,Mwl uliyembania kula mbususu alikuwa ni huyo mkuu wa shule?
 
Hata mimi naliona hili.
Japo hajaeleza kwa kina lkn pia sijaona mahala alipowahi kuonywa kwa barua na mkuu wake kutokana na madai yake ya kujihusisha na mapenzi na huyo mwanafunzi.
 
Asante mkuu, CWT niliwasiliana nao japo mchango wao ni wa kulegalega sana, Upande wa AEK, WEO na TSC ifahamike wote ni tabaka moja lenye uwezo wa kumjadili na kumkandamiza mtu wa chini, na walikaa kikao kabla sijaitwa, ndo maana wakahamisha kutoka kwa AEK kwenda kwa WEO. Hata nilipofika pale walikuwa upande mmoja wa kunilazimisha nikiri kwa madai kuwa wanataka wanisaidie.
Ni askari pekee hakuungana nao huenda kwa vile hakujua hitaji lao.
 
Hilo la kuwa na mkewe walau lina ka uzito fulani. Maana haonekani tena mke wa rafiki kumsaidia kwa lolote wakati yeye ndio wanajuana kuliko hata huyo baba mlezi.
Huenda ni kweli alinihisi hivyo kwa sababu yeye sikuwa namfahamu, na misaada yangu ilijikita kwa yule mwanamke kama mke wa aliyekuwa rafiki yangu.
 
Asante mkuu, nimekuelewa vizuri.
 
Naamini jambo langu lilibadirika baada ya mkuu kujua kuwa jambo lilikuwa linaelekea kwa Katibu tawala mkoa au Baraza la mitihani, lazima alihisi hatakuwa salama kwa uzembe aloufanya. Naamini alinifanyia hivyo kuniziba kauli. Mzazi hakuwa na nguvu kutokana na uelewa mdogo ndo maana mwanae alikosa haki yake ya msingi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…