Dr Msaka Habari
Member
- Apr 9, 2022
- 66
- 32
Na. Mwandishi Wetu, Kigamboni
Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi wilaya ya Kigamboni inalalamikiwa na Mfanyabiashara X kwa kuwatorosha watuhumiwa waliokamatwa na kosa la uharibifu wa Mali na kugeuza kesi ya uharifu wa Mali na kuwa kesi ya mgogoro wa Ardhi.
Akizungumza na mwakilishi wa Jamii Forums Ofisini Kwake, Mjimwema Kigamboni Mfanyabiashara huyo ameituhumu Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Kigamboni kwa kutomtendea haki katika kusimamia mwenendo wa kesi yake na kufanya jaribio la kugeuza kesi ya msingi na kutaka kufanya kuwa kesi ya mgogoro wa ardhi.
"Malalamiko yangu ni kwa Mkuu wa Upelelezi ni juu ya Mkuu huyo kutokutenda haki kwa upande wangu, nimepeleka kesi ya uvunjaji ila yeye na genge lake wanabadilisha kesi wanasema ni kesi ya ardhi, mimi sijapeleka kesi ya ardhi mimi nimepeleka kesi ya uvunjaji nyumba yangu" alisema Mfanyabiashara huo.
Amedai kuwa inakuwaje MTU ambaye hata kiwanja kimoja hana maeneo hayo anakuwa sehemu ya kuratibu uharibifu huo wa Mali na chakushangaza hakuitwa kufanyiwa mahojiano na jeshi la Polisi mpaka tarehe 9/01/2023, baada ya mimi kulalamika ndio wamemuita kumuhoji.
Amesema walikamatwa na Polisi mara tu baada ya kutekeleza zoezi la ubomoaji na Polisi wa Kituo cha Kigamboni na kufunguliwa kesi yenye RB KGD/IR/6640/2022, kesi ya uharibifu wa Mali na kisha kuachiwa kwa maelekezo ya Farid mmiliki wa Simba Oil, lakini mpaka leo sijui kwa nini waliachiwa na hakuna taarifa yoyote mpaka sasa ninayopewa kuhusu mwenendo wa kesi yangu.
Ameongeza kuwa ameshangazwa na kauli ya Polisi kuwa kesi hiyo imegeuzwa kutoka jinai na kuwa mgogoro wa ardhi amesema hajawahi kukubaliana nao toka shauri hilo kufunguliwa licha ya idara ya Upelelezi kupiga danadana kupeleka kesi hiyo mahakamani.
Baada ya malalamiko hayo dhidi ya Idara hiyo ya Upelelezi kikosi kazi kilifanya uchunguzi na kudhibitika kuwa Mkuu wa Idara ya Upelelezi Kigamboni anavinasaba vya maslai na mtuhumiwa namba mmoja ambaye ni mmiliki wa Kampuni ya Simba Oil ambaye ni Farid Salim Mbarak Nahdi.
Tulibaini kuwa kucheleweshwa kwa kesi hiyo ni mpango unaotengenezwa na Idara hiyo kwa makusudi ili kupisha mchakato wa kubadili umiliki wa eneo/Kiwanja plot 23, ili kuhalalisha umiliki wa Bwana Farid kama barua ya Mkurugenzi ya tarehe 15/12/2022 iliyoandikwa kutoa ufafanuzi wa nani mmiliki halali wa eneo/kiwanja hicho.
Pia tuligundua kuwa kesi ya Msingi ni uharibifu wa Mali sasa imekuwaje Polisi kuomba ufafanuzi wa mmiliki halali wa eneo/kiwanja namba 23 wakati Polisi hawana uwezo wa kushughulikia kesi za migogoro ya ardhi.
Baada ya kufanya mahojiano na baadhi ya vijana ambao walishirikiana na Mfanyabiashara huyo kuwakamata waharifu kabla ya Polisi kutokea wanasema walishuhudia gari la Polisi majira ya mchana likiwa na askari ambao walikabiziwa kitita cha fedha na MTU mwenye asili ya kiarabu,
Wanaeleza wakati zoezi la uharibifu wa Mali unaendelea gari la Polisi lilikuwepo maeneo hayo hayo ya tukio kuwalinda vijana waliopewa kazi ya kutekeleza zoezi hilo, kwaiyo hata Polisi walihusika kwenye mpango mzima wa ubomoaji nyumba ya Mfanyabiashara huyo.
Inaripotiwa kuwa tarehe 5/12/2022 waaharifu hao walikamatwa na kufikishwa Kituo cha Polisi, lakini waliachiliwa na kudai kuwa wao walilipwa kwa ajili ya kazi ya kubomoa na hawakujua kama eneo hilo linamgogoro, na walitumwa na MTU mmoja anaitwa Nasri ambaye kimsingi hausiani na eneo hilo.
Kwa upande wake mtuhumiwa alipotafutwa kwa njia ya simu ya Mkononi alikili kufanya uharibifu huo wa Mali na kwamba yeye sio mharifu huku akisisitiza kuwa anachojua kuwa amebomoa nyumba iliyojengwa kwenye eneo lao wanaolimiliki kialali na nyaraka zote za eneo hilo zipo na kwamba X ndio aliyevunja sheria kujenga eneo ambalo sio lake.
"Kinachoendelea kipo katika mikono ya Jeshi la Polisi hayo niliyoyazungumza yanatosha ninachoomba afuate utaratibu aache kunitisha Mkuu wa Upelelezi yupo upande wetu na pia mchunguze habari hizi ili muweze kutenda haki sehemu zote mbili" alisema Nasri.
Naye Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kigamboni amedhibitisha kufahamu jambo hilo na amesema Mfanyabiashara huyo alifikisha malalamiko yake ofisini kwake na alipoona kuna utata alimuelekeza aende kwa RPC Temeke.
Kwa upande wa Ofisi ya Mwendesha mashtaka Kigamboni walisema faili hilo hawalijui na halijafika ofisini kwao hivyo hawawezi kusema chochote kuhusu hilo.
"Tunachoweza kushauri waulizwe walioshika jarada la kesi hiyo uenda wao ndio wakawa wanamajibu mazuri ya kuwapa" alisema afisa mmoja Ofisi ya Mwendesha Mashtaka.