Mkuu wa Wilaya asema "Mkulima atakayekabiliwa na njaa kupelekwa mahakamani"

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Mkuu wa Wilaya ya Mlele mkoani Katavi, Filbarto Sanga, amesema kuwa mkulima yeyote atakayebainika kukabiliwa na njaa atapelekwa mahakamani kutokana na kushindwa kufuata maagizo ya kuhifadhi chakula waliyopewa wakati wa msimu wa mavuno.

Akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi wa msimu wa kilimo 2022/2023 uliofanyika Kata ya Usevya Halmashuri ya wilaya ya Mpimbwe, DC Sanga amesema tahadhari imetolewa mapema kabisa mwanzo wa msimu lakini baadhi ya wakulima wataingiwa na tamaa ya kuuza vyakula vyao vyote bila kuweka akiba ya kutosha.
Filbarto Sanga.jpg

Mkuu wa Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi, Filbarto Sanga

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mpimbwe Catherine Mashalah, ameshauri wakulima kupanda mbegu bora wakati wa mvua za kwanza ili mazao yapatikane kwa wingi.

Kwa upande wao wakulima wamekiri kupokea maelekezo hayo huku wakisema huwa wanauza mazao kwa sababu ya shida zinazowakumba ikiwemo magonjwa na kusomesha.
 
Yupo sahihi saana haiwezekani kushindwa kutambua ni kiasi gani unaweza kutumia kwa mwaka chakula kwenye familia

Ikiwa tunafeli kwa hilo dogo kwenye ngazi ya familia nini kuhusu ukiwa kiongozi utaweza kusimamia matumizi sahihi ya umma .

Tujifunze kutunza bajeti sahihi na ziada inayobaki ndio tuuze ,sio kuuza vyote tuu
 
Mkuu wa Wilaya ya Mlele mkoani Katavi, Filbarto Sanga, amesema kuwa mkulima yeyote atakayebainika kukabiliwa na njaa atapelekwa mahakamani kutokana na kushindwa kufuata maagizo ya kuhifadhi chakula waliyopewa wakati wa msimu wa mavuno.

Akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi wa msimu wa kilimo 2022/2023 uliofanyika Kata ya Usevya Halmashuri ya wilaya ya Mpimbwe, DC Sanga amesema tahadhari imetolewa mapema kabisa mwanzo wa msimu lakini baadhi ya wakulima wataingiwa na tamaa ya kuuza vyakula vyao vyote bila kuweka akiba ya kutosha.
View attachment 2412518
Mkuu wa Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi, Filbarto Sanga

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mpimbwe Catherine Mashalah, ameshauri wakulima kupanda mbegu bora wakati wa mvua za kwanza ili mazao yapatikane kwa wingi.

Kwa upande wao wakulima wamekiri kupokea maelekezo hayo huku wakisema huwa wanauza mazao kwa sababu ya shida zinazowakumba ikiwemo magonjwa na kusomesha.
Hivi watu wa namna hii , hupaje Uongozi, uyu ata yule ambae hakusoma Hata darasa moja anamzidi akili,

Ndo maana nchi ipo ipo tu , huwezi KUWA na watu wa namna hii kwenye uongozi ukawa na serikali imara au taifa bora,
 
Huu ndio uhuru wa maoni mliokuwa mnaulilia awamu ya 5! Kaeni kwa kutulia maana upuuzi uko mwingi bado haujaongelewa tu.
 
Back
Top Bottom