Mkuu wa Wilaya Ilala, ahadi yako ya ukarabati wa hili daraja lini itatimia?

Mkuu wa Wilaya Ilala, ahadi yako ya ukarabati wa hili daraja lini itatimia?

3 Angels message

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2017
Posts
5,350
Reaction score
15,426
Kutokana na athari za mvua zile za mwanzo za mwezi Desemba mwaka jana daraja lililopo eneo la Mwanzo Kata ya kifuru-Kinyerezi lilikatika na kuharibiwa vibaya na hivyo kuleta changamoto kubwa kwa wakazi wa maeneo hayo.

Mkuu wa wilaya ya Ilala alifika kwenye Desemba 17 kujionea athari na kuahidi kuwaleta Tarura waje kutathmini na kujenga daraja la kudumu lakini mpaka leo zaidi ya mwezi hatuoni utimiaji wa ahadi hiyo huku wananchi wakiendelea kuathirika.

Kwa kuona uchelewaji huo waliamua kujenga kivuko cha muda ili kurahisisha angalau uvukaji wa watu ili shughuli za maendeleo zisikwame ila nalo siyo imara sana na lina hatari nyingi hasa kwa watoto.

Tunakukumbusha Mkuu wa Wilaya Ilala ahadi yako itimie ili kuepusha madhara yanayoweza kutokea hasa kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha lakini pia shughuli za maendeleo ziendelee bila kikwazo.

IMG_20211221_124439.jpg
 
Back
Top Bottom