Ninavyo jua mimi Nchi hii inaongozwa kwa Sheria,Kanuni, na Taratibu, nimesikia katika vyombo vya habari kuwa Mkuu wa Wilaya alitoa Amri ya kukatwa kwa Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo kwa madai kuwa alitumia vibaya kalamu yake kutoa maamuzi yaliyo sababisha shamba la mkulima mmoja kuuzwa, Ninajua kuwa Mkuu wa Wilaya husika ndiye Mwenyekiti wa Bodi ya Mahakama ya kushughulikia maswala ya nidhamu kwa Mahakimu wa Mahakama ya Mwanzo. Ina maana Mkuu wa Wilaya huyo hajui kuwa Sheria hiyo ipo na hajui wajibu wake mpaka atoe Amri hiyo ya kumkamata hakimu huyo, au Sheria hiyo imefutwa? na kama haijafutwa yeye amefuata sheria au ametumia mdaraka yake vibaya kwa kujipendekeza ili hapo baadaye ateuliwe tena kuwa Mkuu wa Wilaya.
Ninafikiri kuwa Kauli mbiu ya "Hapa Kazi" haina maana ya kukiuka taratibu,kanuni na Sheria zilizo wekwa. Ninaomba kujua ni hatua zipi ambazo zinaweza kuchukuliwa dhidi ya watu kama ambao wanaoona makosa ya watu wengine wakati nao wakikiuka taratibu na sheria za nchi.