Mkuu wa Wilaya Manispaa ya Tabora analazimisha walimu kuchangia Mwenge na Sherehe za Uhuru

Mkuu wa Wilaya Manispaa ya Tabora analazimisha walimu kuchangia Mwenge na Sherehe za Uhuru

lutelemba

Member
Joined
May 25, 2011
Posts
26
Reaction score
1
Mkuu wa wilaya ya manispaa Tabora mjini ameonja joto ya jiwe baada ya kutaka kuwachangisha walimu mchango wa sherehe za uhuru na mwenge walimu walimuchachafya kwa hoja kwenye ukumbi wa uhadhili mpaka akakimbia.

Anataka akusanye sh 280,000,000 milions kwa ajili ya miaka 50 ya uhuru na mwenge kupitia migogo ya walimu. wanajamii pia tunahitaji mchango wenu hivi ni haki kumchangisha mwalimu kwa ajili ya sherehe za uhuru na mwenge.

Magamba wataimaliza hii nchi.
 
hivi kwa nn tusifute hizi safari za mwenge? zina umuhim gni kwetu zaidi ya kupoteza hela na kutfutia watu posho?
 
Sijui kwa nini kuna watu wanaona umuhimu wa mwenge leo hii 2011, zama za science & technology. Kila kitu kina wakati wake, mwenge umetumika kufikisha ujumbe enzi hizo lakini kwa sasa watu wazima kuzunguka nchi nzima na hiki kibatari ni jambo lisilokubalika. Huu ni uzururaji. Wapeleke hiki kibatari kwenye jumba la makumbusho. huko ndio sehemu stahili na sio kupitisha kibakuli kwa wananchi eti wanataka hela za mwenge! zinaenda wapi hela za mwenge? million 280 kununua mafuata ya taa?
 
Kwa muda mrefu sana walimu wamekuwa wakitumika kama mfuko wa maafa.

Maneneo kama WITO na HAIBA yametumika kuwafanya walimu wapole na wanyenyekevu kupita kiasi.
Upole na Unyenyekevu huo wa waalimu umetumika na watu ambao wala si wapole wala si wanyenyekevu kuwaibia.

Walimu wanapaswa kupinga kunyonywa na kuibiwa kwa nguvu zao zote.
 
Hawa wachangishaji hawaishii kuwachangisa walimu ht mtaani kwa raia wanawachangisha, kn raia wanatoa na wengn wng wanawakimbiza km mbwa koko.
 
Walimu nao wamazidi bana mpaka sasa hawana shirikisho la kueleweka kusimamia haki zao watasimama mmoja mmoja mpaka lini?

Kama wafanyakazi watatetea haki zao kama individual basi wajue serikali itawanyonya kwa miaka mingi ijayo.
 
Yani hiyo sio Tabora tu hata mwanza misungwi walimu wanalazimishwa kuchangia huo mwenge, yani inauma sana kwanini tuendelee kuchangia kitu ambacho hakina manufaa yoyote, mm naona kazi ya mwenge ni kueneza ukimwi na mambo machafu ya pombe. jamani watz tuamke tukatae kukandamizwa na kunyonywa, huo mwenge wangekuwa wanakatwa mafisadi kuliko walimu ambao mshahara wenyewe wanaoupata hautoshelezi kabisa, MFUMO WA SERIKALI ni mfumo wa kinyonyaji kwa wasionacho.
 
unaongelea kwa mt.ko nn? cwt shirikisho la marubani? uliza kwanz
 
Walimu nao wapunguze unyonge duh! Daily wao ni kuonewa na kudhalilishwa teh!
 
Tatizo lenu watanzania hamkumwelewa Jaji Werema. Aliposema tuzuie maandamano alimaanisha tuufute Mwenge ambao ndiyo maandamano pekee yanayokata kilometa nying kuliko ya CHADEMA kwani haya huanzia kona moja ya nchi na kuishia kona nyingine ya nchi.
 
Back
Top Bottom