Mkuu wa Wilaya Maswa aamlisha Uhamiaji wamkamate Mwananchi aliyepewa eneo lake la Mkuu wa Mkoa

Mkuu wa Wilaya Maswa aamlisha Uhamiaji wamkamate Mwananchi aliyepewa eneo lake la Mkuu wa Mkoa

HAKI KWA WOTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2022
Posts
1,108
Reaction score
1,132
Habari,

Muda mfupi uliopita DC MASWA amewaagiza askari wa uhamiaji kumkamata Baraka Kabezi na familia yake yote mkazi wa Marampaka Maswa kuwa siyo raia wa Tanzania na hivi sasa anashikiliwa na ofisi za uhamiaji Maswa.

Chanzo ni mgogoro wa ardhi baina ya Baraka na Diwani wa eneo hilo na DC wa Maswa wanataka nyumba ya Baraka ibomolewe na kupisha njia na siyo nyumba ya diwani iliyojengwa kwenye njia kulingana na ramani ya mipango miji na tayari RC alishalitoa uamuzi swala hili kwa kuagiza nyumba ya Baraka isibomolewe na ramani ya mipango miji iheshimiwe kitu ambacho hakikumfurahisha DC wa Maswa hivyo kumtengenezea tuhuma ya ukimbizi Baraka.

Huu ni uonevu mkubwa na hauvumiliki kwani wazazi wa Baraka ni wenyeji wa Kasulu tangu wazazi wao kwanini na wao wasikamatwe na pia Baraka ana vitambulisho na vyeti vyote vya NIDA na kuzaliwa ambavyo kawaonesha lakini uhamiaji wanataka vyeti halisi baada ya Baraka kuwapatia nakala zilizothibitishwa mahakamani na kuzikataa.

Tunaomba DC huyu achukuliwe hatua kwani anadharirisha nafasi ya uteuzi wa Rais na kukanyaga maamuzi ya RC kwa kujimwambafai.

Nawasilisha kwa hatua sitahiki.
 
Back
Top Bottom