LGE2024 Mkuu wa Wilaya ya Chamwino awapa kazi maalum Wenyeviti CCM / Mabalozi kuhusu uandikishaji

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Mzee wa Code

Member
Joined
Sep 23, 2024
Posts
61
Reaction score
91
Kwa sasa ndio nimeelewa kwanini cheo cha Mkuu Wilaya kinapigwa vita na akitakiwi kuwepo kabisa ni cheo cha kichawa kinachoingiza hasara tu ya kodi za wananchi.

Siku ya jana Alhamisi tarehe 17, 2024, Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Janet Mayanja ameitisha mkutano wa Wenyeviti wa CCM Kata na vitongoji vyote Wilaya ya Chamwino.

Katika mkutano huu DC huyu wa Wilaya alita maagizo kwa Wenyeviti hao kuhakikisha mabalozi wa CCM wote katika Mitaa na vijiji kaika Wilaya hiyo ya Chamwino wanahakikisha wanapeleka majina ya Wananchi wao yakaandikishwe bila hata wahusika kuwepo.

Mkuu wa Wilaya akasisitiza mabalozi wote wanatakiwa kupita kila Nyumba kuwashinikiza wakazi wao wakajiandikishe.

hakuishia hapo Mkuu wa Wilaya aliwataka Wenyeviti hao kupiga kambi katika vituo vya kujiandikishia wao na mabalozi wao ili kukamilisha zoezi hilo la undikishaji, DC Janet Mayanja aliwasisitizia kuwa zoezi hilo ni maalum kwa sababu Wilaya hiyo ndipo ilipo Ikulu, hivyo chama akishindwa kibarua chake kitakuwa matatani.

Kwenye kakao hicho kama kawaida wazee wa CCM wanajulikana kwa kupenda pesa walimuuliza DC anawatuma kazi hiyo wao wenyeviti na mabalozi posho za kuwalipa inakuwaje, Mkuu wa Wilaya bila shaka akawajibu yeye atawalipa posho wote kwa kazi hiyo Kudadadeki.

Nimejifunza kuwa cheo cha Mkuu wilaya ni uchawa wa kisiasa, lakini nilienda mbali zaidi Dc huyu anatoa wapi pesa za kuwalipia posho watu wasiopungua elf kumi posho! Hizi pesa zitatoka wapi na Kwenye Bajeti gani?!

DC au bado una zile pasa za rambirambi ulizokwapua Hanang na misaada wakati wa Janga la Matope, hii hatujasahau pia au ndio umeenza matumizi sasa kwa kulipa fadhira baada ya kupata uhamisho?

 
Hawa wapumbavu naona sasa wameanza kuchakachua kura. CHADEMA wakae chonjo!
 
Ndiyo maana hatuendelei maana nchi imejaa dhuluma.
 
CHADEMA ijitoe kushiriki u haguzi batil.
 
Alafu kavaa kabisa na rozali yaani

Sijui kwanini watu tunapenda sana kumsanifu Mungu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…