Mkuu wa Wilaya ya Dodoma: Viongozi wa Serikali za Mitaa msiwe mawakala wa kuuza viwanja vya wananchi

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma: Viongozi wa Serikali za Mitaa msiwe mawakala wa kuuza viwanja vya wananchi

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wakuu,

Kumbe viongozi wa CCM upande wa serikali za mitaa walikuwa wanauza kiholela viwanja vya wananchi na mlikuwa hamsemi?

Naona CCM sasa wameanza kujiumbua wenyewe hadharani kwa kusema mambo ya hovyo ambayo walikuwa wanayafanya kipindi wako kwenye uongozi.

===========================

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri, ametoa rai kwa viongozi wa serikali za mitaa kuzingatia weledi katika utendaji wao, kuepuka vitendo vya rushwa, na kujiepusha na uuzaji wa viwanja vya wananchi kwa njia isiyostahili.

Aidha, alibainisha kuwa serikali imepanga kutoa mafunzo maalum kwa viongozi hao ili kuboresha ufanisi wao kazini.

Mhe. Shekimweri alitoa tamko hilo JANA, Desemba 4, 2024, katika viwanja vya Shule ya Msingi Dodoma Makulu, jijini Dodoma, wakati akizindua kampeni ya "Nipendezeshe Nisome," ambayo inalenga kusaidia wanafunzi wenye mahitaji maalum kwa kuwapatia sare za shule.

Source: Jambo TV

 
Ukweli mtupu
Kwani kwa kushirikiana na maafisa Ardhi wasio waaminifu wameuza na kujigawia Eneo la Nkuhungu broad acre bila kufuata Sheria
Kwani Eneo lilikwisha tolewa umiliki
 
Back
Top Bottom