SI KWELI Mkuu wa Wilaya ya Hai amepora ofisi ya Mbunge wa Hai

SI KWELI Mkuu wa Wilaya ya Hai amepora ofisi ya Mbunge wa Hai

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Katibu wa Mbunge wa Hai Irine Lema amekanusha uzushi unaozunguka kwenye mitandao kuwa mkuu wa wilaya ya Hai amemnyanganya ofisi mbunge wa hai Mhe. Freeman Mbowe amesema kuwa ofisi ipo Bomang'ombe na imejengwa kwa garama za Mbunge na haiko halmashauri kama inavyopotoshwa

Huu ni Mwonekano wa ndani wa Ofisi ya kisasa ya Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa (CHADEMA) Taifa Mhe.Freeman Mbowe.
1658213820469.png
 
Tunachokijua
Januari 15, 2019, AzamTV kupitia Ukurasa wao wa X (Zamani Twitter) walichapisha video Ikimuonesha aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya akisema Ofisi aliyopewa Mbunge wa Hai, wakabidhiwe Idara ya Uhamiaji kwa kuwa ofisi hiyo haikutumiwa na Mbunge aliyekabidhiwa ofisi hiyo tangu 2010.

Wilaya ya Hai ni moja ya Wilaya iliyoko mkoani Kilimanjaro. Pia Hai ni jimbo ambalo Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CHADEMA alikuwa Mbunge wa Jimbo hilo tangu Mwaka 2000 alipochaguliwa kwa 64.5 ya kura. Hata hivyo alionekana kutoitumia ofisi hiyo tangu 2010 kama alivyotaja aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo kwa kipindi cha kuanzia Julai 28, 2018 hadi Mei 13, 2021.

Akizungumza kuhusu suala hilo Katibu wa Mbunge wa Hai, Irine Lema amekanusha uzushi unaozunguka kwenye mitandao kuwa mkuu wa wilaya ya Hai amemnyanganya ofisi mbunge wa Hai.

Alisema ofisi ya Mbunge, ipo kata ya Bomang'ombe na ilijengwa kwa gharama za mbunge. Ofisi ya Mbunge haikuwa katika Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Hai.
Back
Top Bottom