Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni aingilia taarifa za Madereva wa School Bus kudaiwa kunajisi Watoto

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni aingilia taarifa za Madereva wa School Bus kudaiwa kunajisi Watoto

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Wilaya ya Kinondoni imeanzisha utaratibu wa kuweka Matron katika gari za kubeba wanafunzi, kutokana na kuibuka kwa vitendo vya ubakaji kwa watoto vinavyodaiwa kufanywa na madereva.

Mkuu wa Wilaya hiyo, Godwin Gondwe amesema amepokea malalamiko mengi kutoka kwa wazazi na walezi, wakidai watoto wao kufanyiwa vitendo vya ubakaji katika magari ya shule.

Akizungumza leo Septemba 6, 2022, Dar es Salaam katika Mkutano wa Maofisa Ustawi wa Jamii nchini, Gondwe aliwataka wazazi na walezi kuwa makini kufuatilia taarifa za watoto na kujenga ukaribu, ili wanapokumbana na changamoto waseme haraka.

“School Bus mtoto anapanda wa kwanza anashuka wa mwisho na bahati mbaya wazazi hawafuatilii watoto, hivi karibuni kuna mama alikuja kulalamika mwanaye alifanyiwa ukatili. Dereva alipaki gari akaenda kumfanyia mtoto shambulio la kikatili na mtoto alivyofika nyumbani alikuwa huru kuzungumza na mama,” ameeleza.

Chanzo: Habari Leo

===

Hukumu kwa watuhumiwa soma: Wafungwa maisha kwa ukatili wa mtoto kwenye school bus
 
Kwahio badala ya kuwanyofoa hao madereva na kuwaondoa kuwaweka mbali na watoto popote pale walipo dawa ni kuweka matron kipindi gari linaendeshwa ?

Na wakishuka je au wakati gari limepaki au akiwa anangojea route nyingine ?

Things have Fallen Apart and its no Longer at Ease....
 
Mzazi ushaambiwa hilo, we nenda kalipize kimya kimya, huyo mtu asione jua...

Kuwa kama warusha jiwe gizani...

Haya matendo twayaendekeza sisi wazazi kwa kutegemea mtu akifungwa ndio utaridhika.
Mtu anayemfanyia helpless child anatakiwa auawe au atolewe hata jicho

Tusiwe na huruma kwa wanaoharibu watoto wasio na uwezo wa kuamua
 
Malezi yamekuwa magumu sana siku hizi, hakuna sehemu salama
 
Uko Dar mmekumbwa na balaa gan! mara ndoa nyingi uko uvunjika chanzo wanaume wa Dar kupenda jicho! Gazeti alijafungiwa vitumbua imeibuka tena jingine la kunajisi watoto! Uko si ndyo mitume wote wanapatikana muombewe
 
Kiujumla ni kwamba watu hawana tena ofu juu ya mungu wetu na kwa kuwa tumekosa maarifa basi acha tuu na tunaangamia
 
Kwahio badala ya kuwanyofoa hao madereva na kuwaondoa kuwaweka mbali na watoto popote pale walipo dawa ni kuweka matron kipindi gari linaendeshwa ?

Na wakishuka je au wakati gari limepaki au akiwa anangojea route nyingine ?

Things have Fallen Apart and its no Longer at Ease....
Hujamuelewa DC, yeye kwani anaweza kutabiri dereva fulani atabaka mtoto ?,anachofanya ni kuzuia matukio kutokea mbeleni
 
Na ndio Mana huwa nawaza mno mwanangu nimuandikishe tu shuleni baadaye niwe nampigisha pindi mwenyewe
 
Ushauri wangu madereva wa school bus wawe wakike!
Hata hao wa kike baadhi yao wakiamua kufanya vitendo vya kijinga kwa watoto, watafanya tu. Maana na wenyewe siyo malaika.
 
Hujamuelewa DC, yeye kwani anaweza kutabiri dereva fulani atabaka mtoto ?,anachofanya ni kuzuia matukio kutokea mbeleni
Inabidi yoyote anayedeal na watoto, kukaa karibu nao katika shughuli za kila siku awe amefanyiwa background check, hata kama ni mtu wa hasira, alikuwa jambazi, mlevi au mtu wa shari..., utatuzi sio kuweka mchungaji wa kuwachunga pindi wakiwa kwenye gari.... kama matron ameweza kufanyiwa uchunguzi wakaona anafaa why not dereva ? Au haiwezekani matron ndio akawa bogus kuliko dereva ?

Pili angalizo madogo wengine wakiona jamaa anazingua tu hawachelewi kumzushia jamaa anatukatili
 
Back
Top Bottom