Mkuu wa Wilaya ya Makete amuagiza DED kukarabati vibanda vya stendi ya Makete Mjini ndani ya mwezi mmoja

Mkuu wa Wilaya ya Makete amuagiza DED kukarabati vibanda vya stendi ya Makete Mjini ndani ya mwezi mmoja

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Mkuu wa wilaya ya Makete mkoani Njombe Kissa Kasongwa amemuagiza Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo ndani ya mwezi mmoja kufanya ukarabati wa vibanda vya wafanyabiashara wa stendi ya mabasi Makete mjini pamoja na kuifanya ipitike vizuri wakati wa mvua na jua.

Mkuu huyo wa Wilaya ametoa maagizo hayo Januari 31,2025 alipotembelea stendi hiyo na kufanya mazungumzo na wafanyabiashara wa eneo hilo ambapo amesema muonekano wa vibanda hivyo pamoja na mpangilio wake hauvutii hivyo kwa kutumia mbao hizo hizo ameagiza mtaalamu wa uchoraji ramani kufanya michoro mizuri ya muonekano wa stendi hiyo

ded.png

“Kwa rasilimali tulizonazo hizihizi, sisi Makete Mungu ametubariki ukipita unaona mbao ziko barabarani mbao tunzo tukatafuta wadau, lakini halmashauri lazima wajiongeze tupaboreshe hapa, kwa hiyo natoa mwezi mmoja hapa pawe pamebadilika unanisikia mkurugenzi, uje mchoro mapendekezo katibu wa wafanyabiashara na mwenyekiti wako mtakuwepo kwenye kamati mtafuatilia kila kitu, mapendekezo yote mtashiriki, mnataka mamalishe wakae wapi, ofisi zikae wapi, hapa baada ya mwezi mmoja pawe ni sehemu mpya kabisa, watu wakifika makete wajue ni Makete mpya” amesema Kissa

Amesema stendi hiyo ndiyo inayotambulisha alama ya Makete hivyo muonekano wake ni lazima uendane na hadhi ya makao makuu ya wilaya kwa kuwa na vibanda vya kisasa vya mbao huku akiwaagiza TARURA kufanya matengenezo ya stendi hiyo ili ipitike vizuri muda wote

Source: Green FM
 
Back
Top Bottom