Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Wakati mataifa mbalimbaki dunia yakiadhimisha siku ya wanawake Machi 8, Mkuu wa Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe Bw. Hamad Mbega, ameitumia siku hiyo kuwataka wanawake wenye umri mkubwa maarufu kama “mashangazi” kuacha kutumia vipato vyao zikiwemo fedha za mikopo, kuwarubuni vijana wenye umri mdogo kwa kuwapa fedha hizo kwa lengo la kuwa nao kwenye mahusiano ya kimapenzi.
DC Mbega ameyasema hayo katika viwanja vya Idiwili vilivyopo kata ya Idiwili wilayani humo, wakati akizungumza na wanawake wa Wilaya hiyo walioungana na wanawake wenzao duniani, kuadhimisha Siku ya Wanawake.