DC wa Morogoro Albert Msando amesema anakatwa Tsh. Milioni 2.8 kila mwezi kutoka kwenye mshahara wake wa Tsh. Milioni 3.1 kama rejesho baada ya kukopa Benki kiasi cha Tsh. Milion 106 ili kujenga vibanda zaidi ya 700 kwa ajili ya Wamachinga kufanyia biashara.