KERO Mkuu wa Wilaya ya Ngara anatudhalilisha Watumishi. Achukuliwe hatua!

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mimi ni mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, nina kero juu ya Mkuu wa Wilaya ya Ngara, anaitwa Mathias Kahabi.

Mkuu huyo wa Wilaya ana tabia ya kudhalilisha na kutukana watumishi ikiwa ni pamoja na kuagiza watumishi wawekwe lock up bila kosa lolote.

Watumishi tunanyanyasika sana na tunakosa morali ya kazi kutokana na kudhalilishwa, kutukanwa na mara nyingine kutishiwa kupigwa.

Mara nyingi hujinasibu kwamba yeye ni mwanajeshi hivyo inatakiwa awe hivyo lakini anavuka majukumu yake na anafanya kazi inayotakiwa kufanywa na mkurugenzi mtendaji.

Amesababisha watumishi kuhama kutokana na kuwadhalilisha.

Naomba mamlaka husika zimchunguze na kumchukulia hatua kali iwe funzo na kuleta ufanisi katika utumishi wa umma.
 
Hapa nauona uunngwana wa Tlaatlah
 
Maelezo yako hayajajitosheleza. Unatakiwa kuweka na orodha ya matukio yake yote aliyowafanyia nyinyi watumishi. Na siyo kulalamika tu kwa ujumla.
 
Kwa namna watumishi hasa mlipuko halmashauri nnavyojidhalilisha kwenye chaguzi mpaka mnapelekea taifa kuingia kwenye matatizo kisa kutiki bora huyo mkuu wa wilaya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…