Mkuu wa Wilaya ya Rungwe awakabidhi Maafisa Ugani pikipiki 61 kusaidia Sekta ya Kilimo

Mkuu wa Wilaya ya Rungwe awakabidhi Maafisa Ugani pikipiki 61 kusaidia Sekta ya Kilimo

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Jaffar Haniu amekabidhi jumla ya pikipiki 61 kwa Maafisa Ugani katika Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe ikiwa ni hatua muhimu ya kuboresha na kuongeza tija katika sekta ya kilimo.

Akikabidhi pikipiki hizo, leo Machi 7, 2023, Haniu amewagiza wataalamu hao wa kilimo kwenda na kushiriki ipasavyo katika usimamizi na uzalishaji wa mazao ya kilimo ikiwa ni mbinu bora kuongeza kipato cha kaya na lishe kwa jamii.
Boda.jpg
Aidha, ameagiza pikipiki hizo kutumika kwa malengo mahususi yaliyokusudiwa ikiwa ni nyenzo sahihi ya kuwafikia wakulima kuanzia ngazi ya shina, Kitongoji hadi kijiji.

"Tahadhari msiende kutumia pikipiki hizi kama bodaboda mtakuwa mnakiuka malengo ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kuhakikisha wakulima wanapata ushauri wa kitaalamu na kwa wakati," ameongeza Haniu.

Akishukuru kwa niaba ya maafisa ugani, Jenister Munisi mtaalamu wa kilimo kutoka Kata ya Kinyala amemshukuru Rais kwa maamuzi thabiti aliyoyafanya na kuwa wataenda kutekeleza kwa vitendo zoezi la uzalishaji wa mazao ya chakula biashara kwa ngazi ya kaya na jamii kwa jumla.
Boda Haniu.jpg

Chanzo: MwanaHalisi Online
 
Rungwe Shida Sio Hao Wataalamu Na Pikipiki Tatizo Ni Barabara.
 
Back
Top Bottom