Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Jaffar Haniu akiongozana na Kamati ya Ulinzi na Usalama amefanya ziara fupi tarehe 02.2.2023 katika Hospitali ya Wilaya Tukuyu (Makandana) na kujionesha shughuli za utoaji wa huduma ya matibabu zinavyoendekea sambamba na kuzungumza na wagonjwa.
Akiwa katika wodi mbalimbali amewapongeza wahudumu wa afya kwa kazi nzuri wanazofanya na kuwa kufanya hivyo inaendelea kuwajengea imani thabiti wananchi dhidi ya Serikali yao.
Aidha, amepongeza kwa kasi kubwa inayoendelea ya upanuzi wa hospitali hiyo ambapo jumla ya Majengo mawili yanaendelea kujengwa.
Akitembelea jengo la wagonjwa wa dharura, Haniu amepongeza kwa hatua nzuri ya ujenzi iliyofikiwa na kuagiza fundi anayetekeleza ujenzi huo kumaliza kazi yake haraka ili kuwezesha shughuli za matibabu kuanza kutekelezwa mapema Mwezi wa tatu mwaka huu.
Jengo lingine linalojengwa ni la wagonjwa wa nje (OPD) ambapo lipo hatua ya umwagaji jamvi ghorofa ya kwanza na ujenzi wake unatarajia kugharimu zaidi ya shilingi Billioni Moja.