Tetesi: Mkuu wa wilaya ya Tarime na maandamano ya kujikomba

Tetesi: Mkuu wa wilaya ya Tarime na maandamano ya kujikomba

monjozee

Senior Member
Joined
Sep 19, 2016
Posts
115
Reaction score
297
Taarifa za kiintelijensia (siyo ya polisi) zilizinifikia usiku huu ni kwamba Mkuu wa wilaya ya Tarime Glorious Luoga ameandaa kikundi cha wanaccm toka Tarime Mjini wanaojulikana kwa jina la Naybigena Cooperative ili kuandamana kesho huko Nyamongo kwa lengo la kujikomba kwa rais JPM. Hadi usiku huu DC Luoga bado yupo Nyamongo katika bar moja inayoitwa Wansa akiandaa risala ambayo atasomewa hapo kesho na waandamanaji aliowaandaa mwenyewe.

Maandamano hayo ya wanaccm ambayo wanatarajia kuyafanya hapo kesho katika eneo la *Nyamongo* ulipo mgodi wa dhahabu wa North Mara unaomilikiwa na kampuni ya Acacia yana lengo la kumpongeza Mwenyekiti wa ccm, rais JPM kwa kile Luoga anachodai kuwa ni hatua muhimu za kulinda rasilimali za madini.

Wananchi wanaoishi Nyamongo ambao wamekuwa wakikumbana na madhila ya mgodi wa North Mara wamekataa kushiriki maandamano hayo ya kipuuzi yenye lengo la kumjrnga kisiasa Mkuu wa wilaya mpenda kick.

Wananchi wa Nyamongo na Tarime kwa ujumla hatukubaliani na upuuzi unaopangwa kufanywa na Mkuu wa wilaya hapo kesho kwakuwa bado tuna malalamiko na madai ya msingi ambayo kwa muda mrefu serikali imeshindwa kuyapatia majibu.

Ukiacha hicho kikundi cha kihuni cha ccm, watu wa Tarime hawawezi kumpongeza rais kwasababu wana madai mengi ambayo hayajawahi kupatiwa ufumbuzi ambayo ni pamoja na;

1. Mauaji ya wananchi yanayofanywa na polisi yaliyothibitishwa na kamati iliyoundwa na prof Muhongo wameuwawa watu zaidi ya mia 100 na hawajalipwa fidia.

2. Malipo ya fidia ya ardhi maeneo ya Nyabichune, Mjini kati, Matongo, Murwambe na Nyamichele zaidi ya billion 22 hatujalipwa.

3. Maji hayapo kutokana na vyanzo vyetu kuchafuliwa na sumu ya mgodi na mpaka sasa mgodi haujawahi kutupatia maji safi hivyo kusababisha magonjwa na mifugo kufa mfano Mto Tigite

4. Vumbi la mgodi mawe ya baruti milio ya kutisha. Barabara mbovu. Sisi hatuwezi kuandamana kupongeza chochote kwasababu hakuna hata jambo moja kati ya hayo limejibiwa na makinikia ya rais hasa ukizingatia tulipojaribu kuingia mgodini baada ya rais kusema ni wezi tulikamatwa na wenzetu mpaka sasa wako ndani. Dc acha kutafuta umaarufu wa kijinga.

MASWALI YA MSINGI

1. Je, kwanini maandamano haya yanaandaliwa kwa siri? tena mkuu wa wilaya akiwa baani?

2. Hivi nchi hii serikali si imepiga marufuku mikutano ya hadhara na maandamano? DC Luoga yeye anatoa wapi kibali cha kuyafanya haya ?

3. Je, ni nani anatoa gharama za kusafirisha watu kutoka Tarime mjini kwenda Nyamongo? Na ni kwa manufaa ya nani?

4. Kwanini wananchi walazimishwe kushiriki kwenye maandamano ambayo hawayataki,kwa kuwa kero na vilio vyao vya siku zote mgodini hapo havijatatuliwa?

Serikali hii kwanini inaendesha nchi kwa double standards kwa kiwango hiki?
 
At the end of the day kila Mtu anajikomba Mahali pake. Tunajuana Watz Hasa Wa huko Afrika. Kila Mahali. Hata ungemwona mbowe na Lowassa 2015. Au Lissu na Lema kwa Lowassa huataamini. Kama Hawa ndo wale waleeeeee waleeeeee
 
...Wananchi wa Nyamongo na Tarime kwa ujumla...bado tuna malalamiko na madai ya msingi ambayo kwa muda mrefu serikali imeshindwa kuyapatia majibu...
Nendeni mkalalamike kwa rais wetu kipenzi wa mioyoni Edward Ngoyayi Lowasa.
 
Hamna haja ya kulalamika wakati zile pesa alizosema Msigwa DOLA ZA KIMAREKANI BILLION 700 zinaweza kwenda kutatua matatizo yote ya huko.
Tumwambie rais wetu wa mioyoni Lowasa. Achana na hao akina Msigwa na hizo dola billioni saba.
 
Hicho ndicho kilicho baki, kusema sawasawa na mukulu,
 
Andameni kwenda kumpiga huyo DC. Simpo.
 
Sisi Wakurya si mbhulula kiasi hicho,Mimi nipo nyamwaga siwezi kushiriki huo upuuzi.
 
Taarifa za uhakika ni kwamba amepata aibu ya mwaka ! Baada ya kujikuta kaandamana yeye na familia yake tu .
 
Panapostahili pongezi ni jambo jema kupongeza.

Wivu wa nini?
 
Back
Top Bottom