Mkuu wa wilaya ya Temeke aamlisha watakavaa nusu uchi wachapwe viboko hadharani

Mkuu wa wilaya ya Temeke aamlisha watakavaa nusu uchi wachapwe viboko hadharani

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2012
Posts
4,572
Reaction score
26,885
Source majira

Katika hari inayoelekea kujitungia sheria kulingana na matwakwa ya pande anayoamini yeye either kwa kushauriwa au kwa matakwa binafsi mkuu wa Wilaya Ya Temeke bi Sofia kaamuru maafisa wa vitongoji na wazee wote kuwatandika viboko wale wote watakao vaa nguo amabazo kaziita "nusu uchi" wakati wowote ili kulinda maadili ya kitanzania hasa kwa vijana.

Wazo langu
Hiyo imeanza Temeke tungojee na watawala wa mikoa mingine
 
Ningefurahia zaidi kama tamko hili lingetolewa na "dhaifu" wa nchi ili agizo hili litumike nchi nzima!!

Dada zetu wamezidi aisee!! 'Chapa sana viboko' ila wasije wakawananiii alafu kisingizio kikawa viboko!!

100% nakubaliana naye!!
 
Hajui atendendalo. Yeye awe polisi, mahakama na magereza. Hawa ndio wakuu wa wilaya na mikoa waliopo. Unatarajia kupata maendeleo kweli?
Sina uhakika aliokotwa wapi kabla ya kuzawadiwa ukuu wa wilaya.
 
Sio mkuu wa wilaya ya llala?
 
Akili dhaifu hutoa mawazo dhaifu..
Maadili ya Mtanzania ni yepi kama Rushwa,ufisadi,ulevi wa madaraka ,kujuana kwenye ajira na vimetawala??
Temeke nzima hajaona kero lukuki kwa wananchi zaidi ya mavazi??
Vyeo vya kupeana hiv tab tusubri katiba mpya.
aaaghr
 
Kashindwa hata kusaficha mitaro huko Temeke sasa anakimbilia mavazi!

Na anaamina nini hasa anaposema ya Kitanzania? Temeke inanuka madanguro, au hilo linakubalika kwake?
 
Mkuu, kiswahili naona kinakupa tabu kidogo ,ujumbe wako umefika.
 
fimbo za kuwatandikia kawapatia pamoja na idadi ya viboko na sehemu gani ya mwili itandikwe??
 
Mtoa uzi kaogopa kusema source yake, yap imeandikwa ktk majira ila ww kuna mahala umeisikia kinafiki kabisha umeogopa kuitaja.badili frequency kama huipendi mbona unakomaa nayo.wa aina hyo mpo wengi humu lakin...
 
Hata mia ilianza na moja. Mi namuunga mkono 100% kwasababu imekuwa kero na hapa hili sio suala la imani bali maadili tu. Hivi kwenye zile video za maisha ya Yesu wanawake wanavaa vimini? Hii inaonesha wazi kuwa sasa maadili yamevurugwa sio wakristo au waislam hapa kilichopo ni wote tulisimamie hili.

Tunapozungumzia maadili hapo dini weka pembeni kwakuwa hakuna dini inayokubaliana na upuuzi kama huu. Hebu fikiri;unamkuta dada kavaa kinguo mabega na makwapa yako nje pamoja na kitovu.

Sketi ya kuana na ipo kwenye magoti. Jamani mifano mibaya ni mingi mno. Kwa mifano hii je kuna dini inafundisha waumini wake wavae upuuzi huu? Jibu ni hapana,kwahiyo upuuzi huu wa kuiga kutoka ulaya lazima tuupige vita.
 
Mini nasubiri kusikia kauli ya Wassira, maana hakawii kuhalalisha watu kuchapwa viboko huku akisema ni sehemu ya ibada kwa Waislamu.
 
Unavosema hizi ni nguo fupi unakuwa unaringanisha na nguo ipi ndefu?na ndefu kwa nan?maadili ni rohoni mwako!pia maadili kuvurigika sio kwa dada zetu tu!rushwa inayolalamikiwa bila kuchukua hatua yeyote mbona hawasemi!!acheni dada zetu wajioneshe maumbile yao na wawavutie wanao taka!"inivatation to treaty"mbona wazungu wanaingia nchini wanavaa nguo mbaya kabsa na hawakataliwi!huu ni ubaguzi!
 
Swala la kuvaa ni la mtu binafsi! Akachape kwanza watoto wako uko nyumbani kwake.. Pumbav.
 
Na kwa hakika itafika siku watu watakiri kwa midomo yao kuwa kuna mfumo wa maisha ambao watu wanapaswa kuufuata.
 
Back
Top Bottom