Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 21,741
- 26,735
Kwa miaka sasa wakazi wa Charambe Mbagala maji tunayopewa na Dawasa ni hatari kwa matumizi kwani yana kemikali.
Maji haya yenye rangi ukifulia nguo nyeusi huacha rangi nyeupe kwenye nguo yakaukapo, na ukiyamwaga kwenye mchanga huchukua muda mrefu sana kukauka na yakikauka huacha rangi ya njano kwenye mchanga, na maji haya hutafuna kwa ndani koki za chuma.
Mimi binafsi pamoja na kuwapelekea ushahidi wa maji yao ofisini kwa na kuwaita nyumbani kwangu wayaone maji yanayotoka lakini hakuna suluhisho.
Mkuu wa Wilaya inaelekea maji haya ambayo ni ya kisima si ya kisima kirefu, ni kifupi hivyo tunapata maji yenye harufu na majitaka ya vyoo.
Wengi wa wakazi wameanza kutegemea visima binafsi ambavyo vinachimbwa kwa wingi kutokana na maji ya DAWASA kuwa mabaya.