Mkuu wangu Jokate huyu Mkandarasi mumemtoa wapi?

Mkuu wangu Jokate huyu Mkandarasi mumemtoa wapi?

imhotep

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Posts
55,997
Reaction score
88,219
Kuna Mkandarasi amepewa azibe viraka kwenye Barabara za Temeke ambalo ni jambo zuri sana, kwa sabababu ilishakuwa kero..

Jambo la ajabu kazidi kuyatanua mashimo halafu katokomea kusikojulikana katuachia adha kubwa kuliko hata ilivyokuwa awali.

TARURA nao wanaona freshi tu hela zetu za Tozo kupigwa.

Mkuu Jokate tembelea mtaa Omar Ally Juma na Yombo ujionee.
 
Mkuu wa wilaya asipofika katika hayo maeneo uliyomwambia, basi andaeni maandamano mpaka katika ofisi zake huko Temeke.

Pia piga picha hayo mashimo na kuyatuma katika ma group mbali mbali ya youtube na mitandaoni mingine ili picha hizo ziweze kusambaa haraka na kuwafikia wahusika.
 
Hawa Viongozi wamadhamira nzuri ila katikati yao na sisi Wananchi kuna Wapigaji na Matapeli wa kutisha.

Mkuu nitayapiga picha mashimo nikipita pale.
 
Hawa Viongozi wamadhamira nzuri ila katikati yao na sisi Wananchi kuna Wapigaji na Matapeli wa kutisha.

Mkuu nitayapiga picha mashimo nikipita pale.
Ya ni kweli kabisa, serikali imekuwa ikijitahidi kutatua kero za wananchi kadri inavyoweza kufanya, ila kunakuwa na vibaka uchwara katikati wanaotumia huruma hiyo ya serikali kujineemesha wao na familia zao.

Dawa ni kuwa unawachoma tu kupitia mitandao ya kijamii.
 
Sisi wakandarasi tukipata tenda kabla ya mpunga haujaingia na kutoa ten percent tunaibomoa kwanza barabara ili wananchi mkereke baada ya hapo tunalipwa chetu fasta halafu kazi inaendelea. Endeleeni kupaza sauti
 
Kwaiyo hamna uzalendo sio?
 
Nimeona mashimo yamezibwa kwa viraka vya lami shukurani nyingi kwa wahusika.
👍🏾
 
Tatizo ni upumbavu wa sub contracting ya hizo tender, wanapewa wasio na uwezo na unakuta ni kampuni za kipuuzi tu za viongozi wahuni tu.
 
Kuna Mkandarasi amepewa azibe viraka kwenye Barabara za Temeke ambalo ni jambo zuri sana kwa sabababu ilishakuwa kero..

Jambo la ajabu kazidi kuyatanua mashimo halafu katikomea kusikojulikana katuachia adha kubwa kuliko hata ilivyokuwa awali

TARURA nao wanaona freshi tu hela zetu za Tozo kupigwa.

Mkuu Jokate tembelea mtaa Omar Ally Juma na Yombo ujionee.
Vile vipande alivichukua akaenda kuvitandaza nyumbani kwake.
 
Jokate anaupiga mwingi hata vile viwanja vya Mwembe yanga vinaboreshwa sana.
 
Jokate Please tembelea hizi Barabara za Temeke uone usanii unaofanywa na huyo Mkandarasi inafikia hadi Samia anasemwa semwa.
 
Mkuu sio umesema wameziba👇
Wameziba Mtaa mmoja tu wa Dakta Omar Ali Juma lakini Mtaa wa Ruvuma pale njia panda bado na kueleke Buza nayo nimeona mashimo hayajazibwa wameweka vikokoto vya kisanii
 
Huyu Mkandarasi anamiharibia Mama inabidi Jokate na Mkurugenzi wakomae nae.

Kwanza sio kazi kubwa Mama Samia amapendwa Temeke.

Tunataka siku aje Mwembe Yanga ateme madini.

Tumsikilize bila ya khofu ua kuuwawa na Wasiojulikana.
 
Kesho naenda kuyapiga picha hayo mashimo nije niyaanike humu aibu.
 
Back
Top Bottom