Mkwabi akana kuivuruga Simba

ZionGate

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
6,362
Reaction score
2,991
Wakati wingu na hofu limeendelea kutanda ndani ya Simba kufuatia sintofahamu iliyopo kati ya viongozi na mwekezaji wa klabu hiyo, mfanyabiashara maarufu nchini, Mohammed Dewji "MO", kiongozi mkuu wa mabingwa wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Swedi Mkwabi, ameibuka na kusema naye anashangazwa na hali hiyo iliyopo.

Hofu ya "ndoa" kati ya MO na mabingwa hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba kutaka kuvunjika ilianza kuzungumzwa zaidi ya miezi miwili na taarifa za ndani zinaeleza kuwa hali hiyo imekuja kutokana na kuwapo kwa tofauti kati ya viongozi na mwekezaji huyo wa klabu hiyo ya Mtaa wa Msimbazi, Kariakoo jijini Dar es Salaam.

Hali ilizidi kuwa mbaya baada ya MO kuanza kuandika mfululizo wa ujumbe mbalimbali zenye "mafumbo" katika kurasa zake za kijamii na kuzidisha mijadala miongozi mwa wanachama, mashabiki wa Simba na wadau mbalimbali wa soka hapa nchini.

"Kwenye uongozi, na kwenye maisha, huwa nakaribisha kukosolewa. Lakini siwezi na sikubali kufanya kazi na mtu anayejuhumu malengo, mipango na maslahi mapana ya taasisi, mtu anayetoboa mtumbwi tunaosafiri nao," MO aliandika ujumbe huo katika ukurasa wake huku akiweka picha inayomwonyesha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (kushoto) na kulia ni Mwenyekiti wa Simba, Swedi Mkwabi.

Akizungumza na Nipashe jana, Mkwabi, alisema kuwa hata yeye binafsi haelewi sintofahamu hiyo iliyopo ndani ya klabu yao ambayo kwa sasa iko kwenye mchakato muhimu wa kukamilisha usajili kwa lengo la kuimarisha kikosi chao kwa ajili ya msimu ujao.

Mkwabi alisema kuwa kama kiongozi mkuu, hafurahishwi na hali hiyo kwa sababu haileti "afya" ya maendeleo ya klabu yao na mpira wa miguu hapa nchini.

Hata hivyo, Mkwabi alisema kwamba anasikitishwa zaidi kuona yeye akihusishwa katika sintofahamu hiyo, bila ya kufahamu sababu za msingi.

"Hata sielewi, hata mimi ninashaa, ninatajwa kuhusika kushirikiana na ( majina tunayahifadhi) ili kuzuia mambo yao," alisema kwa kifupi kiongozi huyo ambaye aliingia madarakani katika uchaguzi wa klabu hiyo uliofanyika Novemba mwaka jana chini ya katiba mpya ambayo imempa nguvu mwekezaji asilimia 49 na asilimia 51 zimebakiwa kwa wanachama.

Taarifa za ndani za klabu hiyo zinasema kuwa moja ya sababu ambazo zimepelekea pande hizo mbili kutofautiana, ni kutofanya uamuzi wa pamoja wa mambo mbalimbali yanayoihusu timu yao, ikiwamo suala la usajili wa wachezaji wapya na wale wa zamani, wanaopewa mkataba mipya.

Imeelezwa kuwa, mchakato wa usajili unaendelea klabuni hapo, umesaidia kuwatuliza wanachama ambao wanaamini ujio wa mwekezaji huyo, ulichangia kwa kiasi kikubwa kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara na kufika hatua ya robo fainali ya mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliomalizika.

NIPASHE
 
Nimegundua 80% ya watu wa mitandao yote hata kama wana PhD ni wajinga.
Na komenti moja ya juu hudetamaini ya chini yake mfano mafumbo ya Mo Dewji aliyokuwa akiyaandika mtu wa kwanza kukomenti akiandika pumba basi wote wanaofuata wataandika kwa namna hiyohiyo ni wachache sana huwa tofauti.

Jambo lililopo msimbazi ni kwamba Mo bado hajawa muwekezaji wa Simba japo mashabiki wanaona kama mfumo unafanya kazi na futa kabisa hilo neno lako la kusema Simba sports ina ndoa na Mo.

Bado mpaka sasa Mo hajatoa zile 20B na kuna watu wamezoea upigaji kwenye hizi nyakati za usajili sasa kwa Mo wamechemka usajili unafanyika mkubwa alafu wapigaji hawapigi pesa hawa ndio walioanza kuleta vijimaneno ambavyo si vya kweli.

Mo ni mwenyekiti wa bodi ya Simba na ana shughuli nyingi sana bado hatuna makamu mwenyekiti hivyo anapokuwa kwenye shughuli zingine vikao havifanyiki kuna watu walianza vijimaneno muda mrefu kuhusu hili hadi ikafikia hatua ya Clencet kutaka kujiuzulu lakini Mo akakataa kwa kuwa kaonyesha uaminifu mkubwa.

Na kwa kumalizia kampuni ya Mo juzi tu hapa imesaini mkataba wa kuidhamini Simba sports
 
Mimi huwa ninasema: Simba, Yanga, ni zaidi ya club za mpira.

Huwezi kuingia tu pale kwa kigezo cha kuwa tajiri au mdau wawa michezo
 
Mwambieni awe mpole tu, kama anatatizo alitatue taratibu na sio kwa kumbughudhi Muwekezaji wetu.
Mwambieni hakuna taasisi inayoendeshwa kiurahisi hata Ikulu ni ngumu.
Mwambieni kumpata Mwenyekiti mwingine wa Simba ni kazi rahisi sana hata kesho anaweza patikana. Ila kumpata Mwekezaji sio kazi ya mwaka huu au mwakani au mwaka keshokutwa.
Mwambieni wenyetimu wanataka haya maendeleo yaliyo anza kuonekana katika timu ya Simba yaendelee kuimarika na sio kuzorota.
Mwambie ni bora kwa yeye kujiuzuru kama anaona hawezi kuzikabiri changamoto kuliko kama Mwekezaji atajitoa.
Mwambie tunamtakia kila LA heri mwenyekiti wetu Mkwabi, na bado tunaimani nayeye.
Ajue, No Easy Task.
 
MO anashindwa nini kutengeneza Msimbazi. .wachezaji watambulishwe pale..Umeona wapi Ulaya mchezaji anatambulishwa kwenye ofisi binafsi ya muwekezaji??
 
Wewe na akili yako kweli zero

Simba wana 51 % ,mo 49% harafu account ya simba ina - amount huku wakitaka mo aweke 20bil hata hati hawataki ionekane huu ni ujinga wa mwendo kasi
 
Timu za tz zimejaa wezi tu ,hivi unajua wanapenda kuchangisha ili wale ,hawataki kubanwa na wawekezaji
MO anashindwa nini kutengeneza Msimbazi. .wachezaji watambulishwe pale..Umeona wapi Ulaya mchezaji anatambulishwa kwenye ofisi binafsi ya muwekezaji??
 
Hela za usajiri na mishahara nani analipa?
 
Wewe na akili yako kweli zero

Simba wana 51 % ,mo 49% harafu account ya simba ina - amount huku wakitaka mo aweke 20bil hata hati hawataki ionekane huu ni ujinga wa mwendo kasi
Wewe nyumbu sijakuelewa nini ulitaka kusema?
 
Mo atumbukize mpunga Kwenye chungu aache taraabu mitandaoni.
 
Mwambieni awe mpole tu, kama anatatizo alitatue taratibu na sio kwa kumbughudhi Muwekezaji wetu.
Mwambieni hakuna taasisi inayoendeshwa kiurahisi hata Ikulu ni ngumu.
Mwambieni kumpata Mwenyekiti mwingine wa Simba ni kazi rahisi sana hata kesho anaweza patikana. Ila kumpata Mwekezaji sio kazi ya mwaka huu au mwakani au mwaka keshokutwa.
Mwambieni wenyetimu wanataka haya maendeleo yaliyo anza kuonekana katika timu ya Simba yaendelee kuimarika na sio kuzorota.
Mwambie ni bora kwa yeye kujiuzuru kama anaona hawezi kuzikabiri changamoto kuliko kama Mwekezaji atajitoa.
Mwambie tunamtakia kila LA heri mwenyekiti wetu Mkwabi, na bado tunaimani nayeye.
Ajue, No Easy Task.
 
Wenyè 51% wameweka pesa ngapi?
Wameweka fanbase yenye watu zaidi mln 10,ambao kwa siku watu laki 3 tu kati ya hao mln 10 wakinunua mo ernegy za buku 1 wanamuingizia mo mln km 300 hivi,51% mtaji wao ni watu basi km sio hao watu ndio target ya mo aache mipasho mitandaoni akaanzishe timu yake,amkeni nyinyi mikia
 

Fan base unaithaminisha kwa sh ngapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…