Mkwaju ni nini?

tanga2017

Member
Joined
Apr 30, 2017
Posts
38
Reaction score
56
Huwa nasikia watangazaji wa mpira wakisema Mkwaju wa penalti.

Mkwaju ni nini? Na hivyo kuna mikwaju ya nini na nini.

Karibuni wataalam wa Kiswahili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkwaju ni mti unaotoa tunda za ukwaju. Kama ushawahi kunywa juice ya ukwaju utakua unanielewa.

Hizo maana zingine unazozisikia mitaani sio rasmi.
 
MKWAJU una maana zaidi ya moja.

1.Mkwaju ambao ni mti unaozalisha ukwaju.

2.Mkwaju ni alama mojawapo katika uandishi /

3.Mkwaju ambao maana yake nyingine ni fimbo au bakora
Mfano: Mbao za Mawe alipigwa mikwaju ya kutosa na baba yake.


4.Mkwaju maana yake ni shuti.Wale wanaopenda kuangalia mpira watakuwa wanajua maana ya neno mkwaju.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…