Mkwamo

Mgomo

Senior Member
Joined
May 15, 2019
Posts
174
Reaction score
65
Nasikitika sana kuongea juu ya mpira wa miguu wa Tanzania. vilabu vikubwa nchini simba na yanga Vina zaidi ya miaka 80 vikiongozwa au kuendeshwa kwa mfumo wa wanachama kwa miaka nenda rudi. lakini bado havina miundo mbinu ya kimpira kama vile academy za watoto, vituo vya matangazo (Tv) wala viwanja vya mazoezi halikadhalika na maduka ya jezi za wachezaji ili kudhibiti mapato ya jezi.
Leo Yanga inaitisha harambee ya kuchangiwa ili hali ilikuwa na wanachama mda mrefu lakini bado inakwama kifedha wanachama wanachangia kwa mbwembwe mbele ya kamera mamilioni kwa mamilioni. swali ni je yanga ilipokuwa kwnye ukata wakifedha ilikuwa kwenye mfumo gani wa uendeshaji? na hawa wanachama walikuwa wapi? au nimpka kamera ziwamulike na kupigiwa magoti?
Azam haina hata zaidi ya m iaka 20 lakini kimaendeleo imezishinda club za simba na yanga kimiundombinu japo sio kwa kiwango cha juu japo wameonesha uthubutu.
mfumo wawanachama umetuletea mkwamo wa hali ya juu sana kisoka katika nchi yetu na kutuibulia watu wasio na dira ya mpira na migogoro ya akina Kilomoni na akili Mali mpira wa sasa ni sayansi unahitaji uwekezaji wa hali ya juu na mfumo sahihi wa uendeshwaji usio ruhusu ukanjanja. Napinga mfumo wa wanachama Kwani club zinabaki masikini huku baadhi ya wanachama wakiwa matajiri kuliko club zao na wanachama kuwa na wachezaji wao na kila mwanachama anataka mchezaji wake acheze. (Kocha kupangiwa wachezaji)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…