Mkwara wa Gattuso unamtepetesha Henry na kumuokoa Zambrotta asirudie makosa ya Mwaka 2000…

Mkwara wa Gattuso unamtepetesha Henry na kumuokoa Zambrotta asirudie makosa ya Mwaka 2000…

Gang Chomba

JF-Expert Member
Joined
Feb 29, 2008
Posts
20,649
Reaction score
4,786
Zambrotta alikuwa na Kadi ya Njano, hivyo Thiery Henry alitaka kutumia mwanya huo kumpandisha hasira ili apate kadi nyingine ya Njano na kutolewa nje.

Mara kwa mara Henry alikuwa anapita ubavu alipo Zambrotta na mara kadhaa alijiangusha na akaenda mbali zaidi kwa kugalagala na kuonesha kuwa ameumizwa sana.

Hii haikuwa sawa na sikukipenda kitendo kile.
Mara kadhaa nilishuka na kumsaidia Zambrotta kukaba, na mara zote nilipo shuka Henry alikuwa akinikimbia.

Tuliongea na Zambrotta na kumuonya juu ya Henry.
Pia tukamkumbusha tukio la Nusu Fainali ya Euro2000 dhidi ya Holland ambapo alipewa kadi Nyekundu kwenye dakika ya 36 ya Mchezo.
Tulimuonya pia asimjibishe Henry neno lolote kwa maana anajaribu kumpandisha hasira ili afanikishe kumtoa nje ya Mchezo.

Ilipo fika muda wa mapumziko nilimfuata Henry na kumwambia Cheza Mpira kama Mwanaume, Dunia pamoja na Mkeo zinakutazama, acha kujiangusha angusha kama Binti na kutafuta huruma kwa muamuzi.

Hakunijibu kitu na aliinamisha Kichwa chake chini na kuelekea vyumbani.

Mwishoni wote mnakumbuka tukio alilo lifanya Zidane.
Na alipo kuwa akielekea vyumbani kwa aibu kubwa nikacheka kimoyo moyo na kusema Sisi ni wataliano, tulizaliwa kwanza kisha wajanja wajanja wakazaliwa baada yetu.

Baada ya Mchezo kumalizika tulilipa kisasi cha Euro2000 na Wote tukawa na furaha isio kifani.

Generali Gattuso.

IMG_2646.jpeg


@acmilan_swahili⚫️🔴
 
Aisee simulizi nzuri.
Mpira ulikuwa zamani
 
Back
Top Bottom