Mkwasa atangaza stars, Msuva, Muzamiru, Mnyate nao wachukua shavu

Mkwasa atangaza stars, Msuva, Muzamiru, Mnyate nao wachukua shavu

bryan2

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2016
Posts
3,323
Reaction score
4,679
MKWASA ATANGAZA STARS, YANGA AMUITA MSUVA TU, MUZAMIRU, MNYATE NAO WACHUKUA SHAVU

Sio kweli Yanga Msuva tuu,Vicent Andrew,Haji Mwinyi nao wanatoka Yanga

Lengo la Mwandishi ni nini au ndo kuandika habari Kinazi??

========

muzamiru%2Bsimba%2B2016.jpg

Kocha wa Taifa Stars ametangaza kikosi chake kitakachoivaa Zimbabwe katika mechi ya kirafiki huku Simon Msuva akiwa mchezaji pekee kutoka Yanga.

Mkwasa amewachota viungo wapya ambao wengi wao walionekana hawana nafasi awali.

Mkwasa ameita jumla ya nyota 24 ambao watasafiri kuifuata Zimbabwe Novemba 12, mwaka huu ikiwa ni siku moja kabla ya mchezo huo ulio kwenye kalenda ya Fifa.

Aidha, Mkwasa ameingiza sura mpya kama, fowadi Omary Mponda wa Ndanda, kipa Said Kipao na beki Aidan Michael (JKT) na beki James Josephat wa Prisons na kuwatema masta kama Deus Kaseke, Kelvin Yondani, Hassan Kessy (Yanga), Mwinyi Kazimoto (Simba), Salum Aboubakar, Aggrey Morris (Azam).

Akitangaza kikosi hicho, Msemaji wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas alisema: “Kikosi kitaingia kambini siku moja baada ya raundi ya kwanza kumalizika, yaani Novemba 7 mpaka Novemba 11 kabla ya kusafiri kesho yake kuifuata Zimbabwe.”

MAKIPA:
Aishi Manula (Azam), deugratius Munishi (Yanga) na Kipao (JKT Ruvu).

MABEKI:
Erasto Nyoni, David Mwantika (Azam), Michael (JKT), Vicent Andrew, Haji Mwinyi (Yanga) na Josephat (Prisons).

VIUNGO:
Jonas Mkude, Shiza Kichuya, Mohammed Ibrahim ‘Cabaye’, Jamal Mnyate na Yassin Mzamiru (wote Simba) Himid Mao (Azam) na Abdulrahman Mussa (Ruvu Shooting).

WASHAMBULIAJI:
John Bocco (Azam), Ibrahim Ajibu (Simba), Mbwana Samatta (KRC Genk, Ubelgiji), Elias Maguri (Dhofar, Oman), Thomas Ulimwengu (huru) na Omary Mponda wa Ndanda.

Lucas alisema kutokana na mbanano wa michezo, mechi za viporo Simba vs Prisons, Yanga vs Ruvu Shooting na Mwadui vs Azam, zote zimepangwa kupigwa Novemba 10.

Chanzo: Saleh Jembe
 
Ikiwa kweli basi ujue kocha ana lengo la kuisaidia Yanga kwa kuwachosha wachezaji wa Simba.
 
bryan2
Ashauriwe abadilishe heading yake Sio Msuva Tu au mimi ndo sielewi neno Tu

Ukisoma habari kuna Haji Mwinyi pia Vicent Andrew/Dante wote wanatoka Yanga.
 
Wa Yanga ni Msuva tu jamani maana DEO MUNISH DIDA (kemondo), VICENT ANDREW (faru dume) na HAJI MWINYI ni (abajalo)
 
Wa Yanga ni Msuva tu jamani maana DEO MUNISH DIDA (kemondo), VICENT ANDREW (faru dume) na HAJI MWINYI ni (abajalo)
Michuano yote ya Ndondo cup hajaona hata mchezaji mmoja hata kutoka Kauzu fc tuu...?
 
Back
Top Bottom