Mkwasa atangaza Stars, Yanga aitwa Msuva pekee

Mkwasa atangaza Stars, Yanga aitwa Msuva pekee

RUCCI

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2011
Posts
1,701
Reaction score
1,714
Kocha wa Taifa Stars ametangaza kikosi chake kitakachoivaa Zimbabwe katika mechi ya kirafiki huku Simon Msuva akiwa mchezaji pekee kutoka Yanga.

Mkwasa amewachota viungo wapya ambao wengi wao walionekana hawana nafasi awali.
Mkwasa ameita jumla ya nyota 24 ambao watasafiri kuifuata Zimbabwe Novemba 12, mwaka huu ikiwa ni siku moja kabla ya mchezo huo ulio kwenye kalenda ya Fifa.

Aidha, Mkwasa ameingiza sura mpya kama, fowadi Omary Mponda wa Ndanda, kipa Said Kipao na beki Aidan Michael (JKT) na beki James Josephat wa Prisons na kuwatema masta kama Deus Kaseke, Kelvin Yondani, Hassan Kessy (Yanga), Mwinyi Kazimoto (Simba), Salum Aboubakar, Aggrey Morris (Azam).

Akitangaza kikosi hicho, Msemaji wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas alisema: “Kikosi kitaingia kambini siku moja baada ya raundi ya kwanza kumalizika, yaani Novemba 7 mpaka Novemba 11 kabla ya kusafiri kesho yake kuifuata Zimbabwe.”

MAKIPA:
Aishi Manula (Azam), deugratius Munishi (Yanga) na Kipao (JKT Ruvu).
MABEKI:
Erasto Nyoni, David Mwantika (Azam), Michael (JKT), Vicent Andrew, Haji Mwinyi (Yanga) na Josephat (Prisons).
VIUNGO:
Jonas Mkude, Shiza Kichuya, Mohammed Ibrahim ‘Cabaye’, Jamal Mnyate na Yassin Mzamiru (wote Simba) Himid Mao (Azam) na Abdulrahman Mussa (Ruvu Shooting).
WASHAMBULIAJI:
John Bocco (Azam), Ibrahim Ajibu (Simba), Mbwana Samatta (KRC Genk, Ubelgiji), Elias Maguri (Dhofar, Oman), Thomas Ulimwengu (huru) na Omary Mponda wa Ndanda.
Lucas alisema kutokana na mbanano wa michezo, mechi za viporo Simba vs Prisons, Yanga vs Ruvu Shooting na Mwadui vs Azam, zote zimepangwa kupigwa Novemba 10.
 
NOT ONLY MSUVA BUT ALSO DIDA,VICENT ANDREW AND HAJI MWINYI.

Heading iko wrong sijajua lengo la mwandishi au Unazi nao umechukua nafasi yake nini?
 
Maajabu! Halafu huyo Msuva aliyemtaja kwenye heading ndio hayupo!
 
Mkwasa anatakiwa kufukuzwa , ngoja tumtimue malinzi anayembeba .
 
NOT ONLY MSUVA BUT ALSO DIDA,VICENT ANDREW AND HAJI MWINYI.

Heading iko wrong sijajua leo la mwandishi au Unazi nao umechukua nafasi yake nini?
lengo la mwandishi na sio "leo la mwandishi"
 
Back
Top Bottom